Na Muhidin Amri, Rungwe

WANANCHI wa kijiji cha Lukata wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya,wameipongeza wizara ya maji kupitia wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)kwa kuwaondolea kero ya maji safi na salama iliyokuwepo kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Lukata Uswege Mwakyusa alisema,kabla ya kupokea mradi wa maji,wananchi hasa akina mama walitembea zaidi ya kilomita 1.5 kila siku kwenda kutafuta maji yanayopatikana kwenye milima inayozunguka kijiji hicho.

Alisema,hali hiyo ilisababisha shughuli nyingi za maendeleo kusua sua kwa sababu wananchi walitumia muda wao kwenda kutafuta maji kwa matumizi ya kila siku,badala ya kufanya shughuli za kujiletea maendeleo.

Alisema,hata baadhi ya ndoa zimevunjika na nyingine zipo kwenye migogoro kwa muda mrefu kwa sababu ya wanawake kuchelewa kurudi nyumbani kutoka kutafuta maji.

Mwakasusa,amewapongeza wataalam wa Ruwasa wilaya ya Rungwe na mkoa wa Mbeya kwa kazi nzuri ya kutekeleza mradi huo ambao umesaidia kuokoa ndoa na maisha ya wananchi wa kijiji hicho.

“tunaishukuru sana serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi kwa kutujengea mradi huu ambao ni mkombozi kwa wananchi,sasa wananchi wanapata huduma ya maji kwenye makazi yao na umetimiza kauli mbiu ya Rais wetu mpendwa ya kumtua mama ndoo kichwani”alisema Mwakyusa.

Mkazi wa kijiji Lukata Ngwitia Mwalende alisema, kabla ya kuanza kutumia maji ya bomba mara kwa mara wananchi walikuwa wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo ya matumbo,kichocho na kuhara damu yaliyotokana na matumizi ya maji ambayo siyo safi na salama.


Mwenyekiti wa chombo cha watumia maji ngazi ya jamii(CBWOs)kijiji cha Lukuta Hezon Mwakasusa alisema,hadi sasa zaidi ya watu 290 wameingiza maji ya bomba kwenye nyumba zao.


Alitaja gharama za kuunganisha huduma hiyo majumbani ni Sh.20,000 ambapo kwa mwezi analipa ni Sh.2,000 na watu wanaochota maji kwenye vituo maalum(DPS)wanalipa Sh.1,000 tu.


Aidha alisema,gharama ya kuvuta maji kwenye taasisi za umma zina tofautiana kwani baadhi zinakusanya mapato na zinatakiwa kulipa Sh.200,000 na nyingine kama shule za msingi za sekondari zinachangia Sh.50,000 kwa kuwa majukumu yake ni kutoa huduma.


Mtendaji wa kata ya Kinyala Agness Peter alisema,kwa sasa kijiji hicho kina maji ya kutosha na wananchi wanatumia fursa hiyo kufanya shughuli zao za maendeleo na kuongezeka kwa nguvu kazi.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya Rungwe Moses Mwaisatile alisema,mradi wa Lukuta ulitengewa jumla ya Sh.721 lakini hadi unakamilika fedha zilizotumika ni Sh.milioni 357,391,000 na umetekelezwa kwa njia ya force akaunti.

Alisema,katika mradi huo wamejenga vituo 28 vya kuchotea maji na watu walioingiza maji ndani ya nyumba ni zaidi ya 100 ambao wanaendelea kupata huduma ya maji safi na salama na wanalipia gharama kupitia chombo cha watumia maji kijiji cha Lukata.

Alieleza kuwa,mradi wa maji Lukata unahusisha jumla ya vijiji sita,hata hivyo wameanza na kijiji hicho na vijiji viingine vilivyobaki vitapata maji ya bomba kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

 

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Lukata kata ya Kinyala wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya,wakipata huduma ya maji katika moja ya vituo vya kuchotea maji vilivyojengwa kupitia mradi wa maji Lukata uliotekelezwa  kwa gharama ya Sh.milioni 357,391,000.
 

Mwenyekiti wa kijiji cha Lukata kata ya Kinyala wilayani Mbeya Uswege Mwakyusa kushoto,akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji hicho Ikupa Songela katika moja ya vituo vya kuchotea maji vilivyojengwa katika kijiji hicho.

 

Baadhi ya viongozi wa kijiji cha Lukata na kata Kinyala wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na kaimu meneja wa Ruwasa mkoa wa Mbeya Mhandisi Felix Msangi wa tatu  kutoka kushoto mstari wa nyuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...