Na Said Mwishehe, Michuzi TV

NI Shanwe tu, !Ndivyo unavyoweza  kuelezea baada ya timu ya Soka ya Simba jijini Dar es Salaam kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika kwa kuibuka na matokeo ya jumla ya bao tatu kwa tatu dhidi ya timu y Power Dynamos FC

Simba imecheza na  Power Dynamos FC ya Zambia  katika Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki wa soka ndani na nje ya uwanja huo.

Timu ya Power Dynamos FC katika mchezo huo ulioanza saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza na bao hili lilidumu katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili mchezo ulianza kwa kasi na kila timu ikiisoma timu pinzani na kwa upande wa Simba Kocha alimtoa Jean Baleke na kumuingiza John Boco.

Kuingi kwa Boco kuliifanya Simba kuongeza mashambulizi dhidi ya wapinzani wake Power Dynamos FC lakini walinzi wake walikuwa makini kuzuia mashambulizi.

Hata hivyo kadri muda ulivyokuwa ikienda ndivyo Simba walivyoonesha kuwa wanatafuta angalau bao la kusawazisha  na hatimaye mshambuliaji wake John Boco alifanikiwa kupiga mpira ulioingia wavuni baada ya moja ya walinzi wa Power Dynamos kuugusia mpira huo na kuingia wavuni.

Baada ya Simba kupata bao la kusawazisha kila timu ikawa makini kuhakikisha hairuhusu bao lakini wakati huo huo kuangalia uwezo wa kupata bao la kuongeza.

Hata hivyo hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika matokeo ikawa bao moja kwa moja na Simba imekwenda hatua ya makundi kutokana na matokeo ya jumla .

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Zambia Simba waliifanikiwa kupata mabao mawili akiwa ugenini na Power Dynamos nayo ikipata bao mbili na katika mchezo wa marudiano uliochezaa leo timu hizo zimefungana bao 1-1 na kuifanya Simba kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa.

Kwa matokeo hayo Simba  inaungana na watani wake wa jadi Yanga ambao tayari wameingia hatua ya makundi baada ya kupita miaka 25 kwani mara ya mwisho iliingia hatua hiyo mwaka 1998.

Hata hivyo katika mchezo wa Simba na Power Dynamos  ulikuwa umetawaliwa na mbinu nyingi za mchezo na hivyo kusababisha makocha wa timu zote mbilii kuusoma mchezo huku wakibadilsha wachezaji kulingana na mbinu  za kupata matokeo kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...