Iringa

Timu ya Mpira wa miguu ya TARURA yaendeleza ubabe kwa siku tatu mfululizo ambapo Leo imefanikiwa kuipiga Ardhi goli 1-0 kwenye mashindano ya SHIMIWI.

Katika mchezo wa Leo uliochezwa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Mkwawa,TARURA ilifanikiwa kuona goli la ardhi katika kipindi cha kwanza dakika ya 28 ambapo mchezaji Erick Tegamaisho aliipatia goli la ushindi.

Hadi mwisho wa mchezo huo timu ya Ardhi haikufanikiwa kuliona goli la TARURA licha la mchezaji wa TARURA Makunge Mwera kupewa kadi nyekundu.

Hadi Leo TARURA inaongoza kwa kuwa na point 9 na magoli  8 ambapo katika mechi ya kwanza dhidi ya Wakili Mkuu iliibuka kidedea kwa magoli 4-0 na katika mechi ya pili dhidi ya Wizara ya Elimu ilitoka mshindi kwa 3-2.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...