Na Humphrey Shao,Michuzi TV

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) linaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Boti za uokozi katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa.

Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema wanaendelea na utekelezaji wa ujezi wa boti hizo tano za uokozi ambapo mbili zitakuwa ziwa Victoria, mbili Ziwa Tanganyika na moja Ziwa Nyasa.

"Tunatekeleza ujenzi wa boti tano za uokozi ambapo tunataka tuweke pale ziwa Victoria boti mbili, ziwa Tanganyika mbili na pale ziwa Nyasa boti moja, taratibu zimeshaanza kuangalia uwezekano wa kufanya vitu hivyo ili baadae tufike mahala tuweze kuwa na boti hizo za uokozi ambazo zitakuwa tayali kukimbia katika maeneo ya matukio kwenye maeneo ya karibu.

"Kutekeleza mradi wa kimataifa wa mawasiliano na uchukuzi katika ziwa Victoria, ambao ni mpana sana lakini lengo lake ni kuboresha mawasiliano na pitia itasaidia katika shughuli za uokoaji zinapotokea ajali watu waweze kuwasiliana na msaada wa karibu uweze kufika, ziwa letu ni kubwa kubwa katika eneo tunalolimiliki, mradi huu umelenga kuwasaida watu wa kawaida kabisa, kwaiyo Serikali imeenda chini hata kuwafikiria watu wa chini." Amesema Mlali na kubainisha kuwa .

"Tumefanikiwa kuongeza dhambuni za meli za kigeni, dhabuni hizi kazi kubwa sana ni kuhakikisha usalama kwa sababu kama vyombo vinakuja lazima tuvikague vizuri alafu vikitoka katika bandari zetu vikapata hitilafu ambayo inaelezeka itaonekana kwamba hatukuwa makini katika ukaguzi, kwaiyo tunakagua na kutoa taarifa ambazo zinaheshimiwa katika bandari zile meli zinaenda.

"Tumefanikiwa kuongezea kwa mchango katika mfuko wa serikali, hii naomba muiangalie vizuri sana, ni taasisi changa imeanza kama miaka mitano iliyopita lakini naomba muone huu muuendelezo wa uchamgiaji katika mfuko mkuu wa Serikali, nadhani msajili wa hazina ni shahidi katika hili, tumetoka milioni 9 lakini sasa tunazungumzia 43 ni ongezeko kubwa sana  kuchangia mfuko wa serikali."amesema.

Amesema mafanikio mengine ni kama kusimamia kudhibiti huduma za bandari baada ya ulasimishaji wa bandari 20 zikiwemo bandari bubu ambapo usalama wa watu, usalama wa vyombo lakini pia hata usalama wa mazingira.

"Tunaendelea kusimamia utekelezaji wa mikataba na miongozo mbalambali kama nilivyoeleza, sisi tunafanya biashara za kimataifa basi tupo katika kutekeleza matakwa na mikataba tuliyoingia ya kimataifa pia.

"Tasac tunatoa leseni, kuzihuisha na kufuta kwa wale ambao wanakuwa wameshindwa kutekeleza matakwa na taratibu za viwango vinavyodhibitiwa.

"Lengo ni kuzifanya bandari zetu ziweze kupata sifa nzuri Duniani, lakini pia tunaweka masharti yanayo dhibiti tozo miongoni mwa watoa huduma kuweka usawa wa ushindani ili ktutoharibiana Biashara."

Katika hatua nyingine amesema"Tunasimamia mienendo ya watoa huduma katika sekta na kutoa taarifa kuhusu nafasi masuala mbalambali yanayohusu majukumu ya shirika.

"Naomba nieleze mafanikio yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana kama ifuatavyo, kwanza tukefanikiwa kuongeza idadi ya kazia kutoka 6000 mwaka 2020 hadi zaidi ya kazia 10'000 mwaka 2021/22 hapa ninaomba tu muone kwamba ndani ya kipindi kifupi lakini uhuduumiaji kazia umekuwa na mafanikio kwa idadi inavyojieleza.

"Lakini pia tuemefanikiwa kuunda nyenzo ambazo zina dhibiti, nyenzo hizi ni pamoja na kanuni na miongozo mbalambali ili ziweze kuongoza na kuleta nidhani katika sekta yetu ya usafiri wa maji, lengo ni sekta yetu ya usafiri maji iweze kwa salama."

Hakuishia hapo amebainisha kuwa  "Tumeongeza idadi ya watoa huduma wanao dhibitiwa na Tasac kwa maana ya idadi ya leseni na  vitu vya usajili vilivyotolewa, kwani majukumu mjowapo ni kutoa leseni na kusajili meli za ndani na za nje, iidadi ya leseni zimekuwa zikiongezeka.

Amesema wamfanikiwa kuongeza idadi ya mabaharia, na hata uelewa wa namna gani usafiri wa maji unatumika kwa Wananchi, huku idadi ya vyombo vidogo ikiongezeka kwa wahusika kujisajili na kutambulika, kuongezeka kwa mapato ya serikali na wataalamu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...