MKURUGENZI wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA ZNZ) Dkt. Mzuri Issa amesema kuwa ni muhimu kuwa na sheria nzuri za habari ambazo zinapelekea kuwepo kwa uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza kwa jamii.
Amesema hayo wakati wa mkutano wa kutoa mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya tume ya utangazaji ya Zanzibar (No. 7, 1997), ambao uliwashirikisha kamati ya masuala ya habari (ZAMECO), asasi za kiraia na tume ya kurekebisha ya sheria uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali Mazizini Zanzibar.
Dkt. Mzuri aliongeza kuwa ipo haja ya kufanyiwa marekesbiso sheria hiyo ili kutoa fursa ya uhuru wa kujieleza ambao ndio chanzo kikuu cha maendeleo ya nchi.
“ Uhuru wa habari na haki ya kupata habari pamoja na uhuru wa kujieleza ni mambo ya msingi katika maendeleo ya nchi na inaleta hata furaha ya mtu binafsi”, amesisitiza Dkt. Mzuri Issa, katika mkutano huo wa siku moja ulioangaliwa na ZAMECO kufuatia hatua ya Tume ya Mabadiliko ya Sheria kuipitia sheria hiyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria Zanzibar, Ndugu Khadija Shamte amesema kuwa muda umefika sasa kuwa na sheria zinazokwenda na wakati na tume iko tayari kushirikiana na wadau kwenye kupokea maoni ya kurekebisha sheria ili kutoa fursa kwa vyombo vya habari kukua na kuwa na ushindani katika kusambaza taarifa.
“Tunahitaji kushirikiana kwa pamoja na mwisho kupata sheria bora na nzuri ambayo italeta mabadiliko katika tasnia ya habari Zanzibar”, Khadija Shamte, M/kiti Tume ya Kurekebisha Sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...