WANAUME nchini wametakiwa kufahamu masuala ya afya ya uzazi ikiwemo masuala ya uzazi wa mpango na siyo kuwaachia wanawake pekee ili kuondokana na mimba zisizotarajiwa.
Akizungumza na waandisha wa habari hivi karibuni Jijini Dodoma Daktari Robert Shokolo kutoka Shirika la Marie Stopes(MST) amesema pamoja na kujikita katika haki sawa kwa wote bado kumekuwa na mfumo dume katika ufahamu wa masuala ya afya ya uzazi kwa wanaume.
Amesema kuwa kuna baadhi ya wanawake wanakwenda kliniki kwa ajili ya uzazi wa mpango lakini ukiwashauri wanasema mpka wakashauriane kwanza na wenza wao
“Ni muhimu sana kwa wanaume kushiriki masuala ya afya ya uzazi,kufahamu njia za uzazi wa mpango,ujauzito pamoja na mambo ya kujifungua kwa sababu ni moja ya watu wa muhimu sana katika kuhakikisha wenza wao wanapata huduma sahihi,”alisema Dkt.Shokolo.
Alisema miongoni mwa madhara makubwa yanayoweza kutokea ni pamoja na ongezeko la mimba zisizotarajiwa hivyo ni vyema wapenzi,Wenza na familia wakawa na familia ambayo wanaihitaji kwa wakati huo.
Sasa kama ikiwa jamii au vijana haitapangilia masuala ya afya ya uzazi ni rahisi sana kupata mimba zisizotarajiwa na hata kujipanga kiuchumi inaweza kuwa ni changamoto,pamoja na kupata magonjwa ya zinaa.
Pia,Dkt. Shokolo ameshauri vijana balehe wapewe elimu ya afya ya uzazi mapema ii kuweza kupangilia na kujikita katika majukumu mengine na kuondokana na changamoto ya mimba za utotoni hasa kwa wasichana.
Dkt.Shokolo alisema mwaka jana zilitoka takwimu kutoka TDHS-(Tanzania Demographic and Health Survey)na zilieleza kuwa asilimia 22 ya vijana kuanzia miaka 15-19 walishawahi shika ujauzito hivyo kundi hilo ni muhimu sana kupata elimu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...