Na Jane Edward, Arusha
WANAWAKE wameshauriwa kuondoa mfumo tegemezi unaowarudisha nyuma kinaendeleo, badala yake wajenge tabia ya udhubutu, itakayosaidia kuwaimarisha kiuchumi ndani ya familia zao na taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Beth Mkwasa wakati alipokuwa kwenye maadhimisho ya kila mwezi ya kusemezana kwa wanawake wakatoliki Tanzania (WAWATA) wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, katika Parokia ya Moyo Safi wa Bikra Maria,Ungalimited jijini Arusha.
Mkwasa ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na mwandishi wa habari mwandamizi mstaafu, alisema Tanzania imejaliwa kuwa na wanawake wengi wenye nguvu na taifa linawategemea, lakini wengi wao bado wanaishi kwa mfumo wa utegemezi.
Alisema akina mama vizuri sasa wajitambue na kuachana na mfumo wa kiafrika wa utegemezi na kujiajiri wenyewe kwa kuanzisha biashara ndogo,.
"Akna mama vizuri sasa mkaachana na utegemezi wa wanaume, sababu wenhi wanaofabya hivi mwisho wa siku maisha yao yanaishia oabaya na kushindwa kulea familia hasa pale baba anapoyumba kimaisha au anapofariki,"alisema.
Awali Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Bikra Maria, Padri Festus Mangwangi alisema WAWATA wamekuwa na desturi ya kusemezana, ili kukumbushana wajibu katika kutekeleza majukumu yao na kujiweka kando na mambo yasiyompendeza Mungu.
Aidha, aliwahimiza watu kupenda kwenda kwenye nyumba za ibada, ili kufafanuliwa neno la mungu na jijsi gani ya kuishi ili mioyo yao iwe na hofu na mungu .
Akiwataka wanawake katika kusemezana kwao wahakikishe wanawajibika ipasavyo katika kulea familia na kutunza ndoa zao, wazingatie maagano ya ndoa na kuepuka michepuko na mambo yasio faa kwenye ndoa.
"Leo Dekania ya WAWATA Jiji Mashariki yenye parokia 11 na vigango vyake ,wamekusanyika katika parokia ya moyo safi Ungalimited, kwa ajili ya kusemezana na walichagua mada isemayo mama mkatoliki na imani katoliki, kuitunza, kuitetea na kuisambaza, "alisema.
Alisema mwanamke anawajibu wa kushiriki maendeleo na kuhudumia familia kama shamba la mzabibu pasipo kumtegemea mwanaume.
Padri Mangwangi alisema kila mwanamke anawajibu wa kushiriki shughuli za kiuchumi na kuondoa mfumo wa kiafrika wa kumtegemea mwanaume akafanye kazi.

Mwenyekiti wa WAWATA jimbo hilo, Bakhita Manga alisema utaratibu wa kusemezana kwa akna mama wakatoliki, kumesaidia kujenga utume wa kujitolea , malezi, kujitambua na kufundishana .
" Utaratibu huu wa kusemezana kumesaidia kuwajenga kiimani na mwanamke kutambua wajibu wake na namna ya kushiriki katika maendeleo ya kifamilia na Taifa,"alisema

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...