Na Jane Edward, Arusha

Wilaya ya Karatu imefanikisha kujenga barabara za kiwango cha lami zenye kilometa 2.8 kati ya mtandao wa barabara wenye kilometa 712 kwa ajili ya kuupendezesha mji huo na kuwa mvuto kwa watalii wanaofika katika wilaya hiyo.

Akiongea wakati wa ziara fupi kutembelea barabara Mjini Karatu Meneja wa Tarura wilaya ya Karatu Mhandisi Msetu Madara amesema ikiwa ni Siku ya mwisho ya Kikao Kazi cha Tarura Mkoa wa Arusha wanashukuru Rais Samia kwa kuleta fedha sanjari na Mkuu wa Wilaya hiyo Dadi Kolimba kusimamia fedha hizo na kutoa ushirikiano hali inayofanya kazi kuwa rahisi.

Amesema kama wanavyojua mji huu ni kitovu cha Utalii na wanataka upendeze na vilevile katika jitihada za kumuunga mkono Rais Dkt.Samia baada ya ile filamu ya The Royal tour ambayo kimsingi kwenye lango la Utalii kuelekea kwenye vivutio ambapo wameona watalii wamefurika hivyo lazima kuboresha miundombinu ya barabara ili watumiaji waweze kufurahia.

"Ili kuongeza mtandao huo Tarura wilayani humo kwa Leo tumetembelea kuona km 2.2 za lami ambazo zimejengwa katika kipindi kifupi cha awamu ya Sita, lakini pia tunaendelea na ujenzi wa madaraja, makaravati,vivuko, katika maeneo korofi wilaya nzima kwa ujumla Hadi Sasa tumefanikiwa"Alisema Mhandisi Madala

Kwa mujibu wa Mhandisi Madara amebainisha kwamba baada ya Ukaguzi wao wameweza kubaini makaravati 296 na madaraja 21 ambayo wameweza kuyajenga kwa nyakati tofauti huku akitolea mfano wa daraja Kubwa lenye upana mita 7 ambalo limeondoa adha kwa wananchi wa eneo la kijiji cha Endamariek

Hata hivyo amesema wameweza kujenga madaraja mbalimbali kwa siku za karibuni eneo la njiapanda Tutsi kwa kutumia Teknolojia ya mawe na kutumia takribani million 32 na eneo la Marera Kilimatembo pamoja na eneo la Sabasaba Mbulumbulu ambapo madaraja hayo ni gharama nafuu na imara ambayo yatawasaidia wananchi.

Amesema wanaendelea kutumia Teknolojia hiyo katika kuhakikisha kwamba wanaboresha maeneo ambayo yana changamoto ya vivuko ili wananchi waweze kupata huduma stahiki ikiwemo Tahadhari za mvua za Elnino.
 
"Kimsingi tumeweza kutumia zaidi ya shilingi billion 2.37 kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 na kiasi hicho hicho cha fedha tunaenda kutekeleza miradi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa hiyo tunaamini sehemu yeyote tutaenda kuitendea vyema na mitaro mingi inapitika japo Kuna baadhi ya wananchi ambao wanaendelea kutupa taka baadhi ya maeneo"Alisema

Akitoa wito kwa wananchi wilayani humo amesema kuacha tabia ya kutupa taka katika mitaro hususani baadhi yao katika maeneo yao ya Kazi mbele ya ofisi zao waache nao wataendelea kutoa Elimu kupitia kurasa mbalimbali.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...