Na Pamela Mollel,Arusha
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kimepongeza waandaaji wa mbio za Mount Meru Marathon Kwa kujitolea vifaa mbalimbali kusaidia Uzazi Salama kwa wakinamama wasio na uwezo wa kununua vifaa vya kujifungulia.
Akiongea Mara baada ya kuwakabidhi vifaa hivyo katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na kuzindua Bonanza hilo linalotarajiwa kufanyika siku ya 9Desemba 2023 (kesho) katika viwanja vya Ngarenaro
Katibu wa itikadi na Uenezi Mkoa wa Arusha Saipulan Ramsey amesema Mount Meru Marathon imeonyesha kuunga Ilani ya chama cha mapinduzi CCM.
Amesema katika Ilani yao ukurasa wa Tano inaeleza kuimarisha huduma za mama na mtoto na hivyo kuchukua hatua ya kuwapongeza kwa kugusa ibara ya 8 ukurasa 5 ikiwemo mazingira mazuri ya mtoto kuja Duniani
Kwa Upande wake Mwanzilishi wa Mount Meru Marathon Sports Promotion Dinnah Mushi amesema Lengo la bonanza hilo ni kuwanyanyua vijana wote nchini kuona jinsi gani wanavyoweza kujitambua pamoja na kusaidia mama anayejifungua na vifaa vyote vikiwa salama.
Awali akiongea Afisa ustawi wa Jamii hospitali ya Mount Meru Teresia Constantine amewashukuru sana Mount Meru kwa vifaa hivyo akieleza vitatumika kwa wagonjwa watakaojifungua Leo na vitakavyobakia watavitumia kwa kinamama wengine.
Naye Meneja wa Tawi wa Benki ya KCB Oprah James ambao ndio wadhamini wakubwa wa Mount Meru Marathon wameeleza kuguswa kwa tukio hilo la kutoa vifaa vya kujifungulia kwa kina mama kwao wakiwa kama wadau wa maendeleo wataendelea kujitolea kurudisha faida kwa Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...