Na Pamela Mollel,Arusha

Wakati Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori nchini(TAWIRI) ikieleza mapito ya wanyama(shoroba)  41 yapo hatarini kufungwa kutokana na ongezeko la shughuli za kibinaadamu ,Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange ameonya viongozi wa vijiji wanaohamasisha uvamizi wa maeneo hayo.

Maeneo ya mapito ya Wanyama ni muhimu katika Utalii,  uhifadhi na kibaiolojia kwa Wanyamapori  kwani ndio yanatumiwa na wanyama kutoka eneo moja kwenda jingine kutafuta malisho ,uzao mpya na kujilinda na magonjwa.

Akizungumza na waandishi wa habari,Mkurugenzi wa Utafiti wa TAWIRI Dk. Julius Keyyu alisema maeneo ya shoroba 41 nchini, ikiwepo eneo muhimu la shoroba ya kwa kuchinja wilaya ya Babati yapo hatarini.

Dk Keyyu alisema, kuna Shoroba 61  katika maeneo mbali mbali nchini, 20 tayari zimejifunga na hivyo bila hatua za haraka kuchukuliwa tatizo litakuwa kubwa zaidi.

"Jambo ambalo Tunaliomba ni kulindwa Shoroba hizi na vijiji, kwa kuhakikisha vijiji vinakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, kwa kutenga maeneo ya wanyamapori, maeneo ya makazi, kilimo na shughuli nyingine za kijamii"alisema

Alisema hivi sasa shoroba muhimu zipo hatarini, ikiwepo shoroba ya kwa kuchinja, ambayo ipo kati kati ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Manyara.

"Ambacho hadi sasa kinasaidia kutofungwa kabisa Shoroba hii ni uwepo wa hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Burunge na tunawashukuru sana walioanzisha hifadhi hii kwani bila wao nadhani hali ingekuwa mbaya zaidi"alisema

Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange, akizungumzia jitihada za kulinda uhifadhi ikiwepo mapito ya wanyamapori, aliwataka viongozi wa vijiji  vinavyounda Burunge WMA  wanaochochea migogoro kuacha mara moja.

Twange akizungumza na viongozi wa kijiji cha vilimatatu moja ya vijiji vinavyounda Burunge WMA, alisema  serikali inajua kuna baadhi ya viongozi waliopo madaraka na wastaafu, wanachochea migogoro katika eneo hilo kupinga  shoroba kwa manufaa yao.

"Wewe kama kiongozi unaona huwezi kusimamia mipango ya serikali kuendeleza uhifadhi na kulinda Shoroba basi bora uachie ngazi lakini serikali lazima itachukuwa hatua kwa wachochezi wote"alisema.

Katika kijiji hicho, hivi karibuni wananchi  waliandamana na kufunga ofisi za serikali ya kijiji cha vilima vitatu, wakipinga kuwekwa alama za shoroba katika maeneo yao.

Waziri wa maliasili na Utalii, Angella Kairuki, akizungumza  katika kongamano la 14 la Wanasayansi, lililoandaliwa na taasisi ya wanyamapori(TAWIRI) alitaka kulindwa kwa maeneo 41 ya Shoroba nchini ili kuendeleza uhifadhi na Utalii.

Alisema Shoroba 20 tayari zimejifunza kabisa na hivyo serikali inafikiria kuziondoa katika orodha na hivyo kubaki Shoroba 41 tu katika maeneo mbali mbali nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...