*Aokolewa
*Kisha ajifungua Salama

MWENYEKITI wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda na msafara alioambata nao wamejikuta katika Simanzi nzito mara baada ya kumuona Mama aliyejifungua saa chache mara baada ya kuokolewa kwenye tope ambalo lilikuwa limemuenea mwili mzima na kumsomba mita kadhaa.

Akizungumza leo  Novemba 06, 2023 alipomtembelea Mwanamke huyo katika Kituo cha Afya Gendabi mahali ambapo ndipo kulikuwa na maafa kufuatia mafuriko yaliyotokea mara baada ya Mlima Hanang Mkoani Manyara.

"Nimeshindwa kujizuia mimi kama Mama nikajikuta nalia kwa uchungu kuona Mwanamama huyu ambaye alisombwa na tope na kuweza kuokolewa kwenye tope hilo na kufikishwa hospital masaa mawili baadaye kujifungua salama

Mtoto wa kiume Desemba 03, 2023 kwa kweli nimelia uchungu baada ya kusikiliza simulizi za Mama huyu namna alivyohangaika kuokoa watoto wake wawili na huku mjamzito wa miezi tisa hakika hakuna kama Mama. Namshukuru sana Mungu kutenda maajabu na kumuwezesha mama huyu kujifungua salama na mtoto yupo Salama na ameitwa Mussa ."

Aidha Mery amesema Jumuiya itafanya jitihada kuhakikisha wanamuongezea mahitaji ya kutosha.

Mama huyo ambaye kwa sasa yeye na familia wanalala hospitali kutokana na kukosa Makazi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya kutokana na mafuriko ya matope yaliyoikumba baadhi ya maeneo ya wilaya ya Hanang.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...