Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda ameongoza na  Kundi la wanawake  wa Jumuiya hiyo  kwenda  kukabidhi zawadi  kwa Mama aliyejifungua mara baada ya  kutolewa  kwenye  tope.

Akizungumza  leo  Mara baada ya Kukabidhi Vifaa hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema UWT  imeamua kurudi tena kuja kukabidhi Nguo za mama  , mtoto mchanga na mabinti wawili wa mama huyo ambae ni wahanga mara baada ya kuona kuwa anahuhitaji wa haraka hili kuweza kumsitiri mama huyo na watoto wake.

"Leo tumekuja  na magodoro, Blanketi, shuka, Nguo za Mtoto, nguo za Mama, nguo za watoto wa kike waliookolewa mabeseni, fedha taslimu laki sita na ishirini pamoja na mahitaji mengine ambayo yatamsaidia  kuanzia maisha  kwa sasa “amesema Chatanda 

Aidha katika  Msafara huo wa Mwenyekiti Chatanda ameongozana na Wadau  wa Maendeleo Husein Gonga ambae ametoa Bati 50 kwa ajili ya Mama huyo ajengewe nyumba  na ahadi mbali mbali kutoka kwa Wabunge wanawake walioambatana nae .
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...