Na Issa Mwadangala.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista
Mallya Disemba 29, 2023 ameendelea na operesheni ya ukaguzi wa magari ya
abiria kwenye barabara ya kwenda Mbeya Tunduma katika kituo cha ukaguzi
wa magari Mahenje wilayani Mbozi.
Katika opereshion hiyo kamanda
Mallya amemfutia leseni dereva Ally Lugenge (56) akiwa anaendesha gari
lenye namba za usajili T855 DXL Kampuni ya Masihi inayofanya safari zake
Ubaruku-Mbeya-Tunduma na Ileje.
Gari hilo aina ya Fuso yenye
uwezo wa kubeba abiria 45, ambapo kondakta na dereva wa gari hilo
walipakia abiria zaidi ya 66 pamoja na mizigo kitu ambacho ni kinyume na
taratibu za sheria za usalama barabarani pia ni hatari kwa usalama wa
abiria.
Kamanda Mallya amechukua uamuzi wa kumfutia leseni dereva
huyo baada ya kurudia kosa ambalo alilifanya jana la kuzidisha abiria
ambapo alipewa onyo kali kisha kutozwa faini lakini dereva huyo alirudia
kosa lilelile ambalo lilimpelekea Kamanda Mallya kumfutia leseni dereva
huyo.
Sambamba na hilo Kamanda Mallya amewakamata makondakta
wawili wa mabasi madogo ya abiria kwa kosa la kuchanganya abiria na
mizigo kwenye gari la abiria ambalo ni kosa kwa sheria za usalama
barabarani, makondakta hao ni Frank Dicksoni (24) pamoja na Zakayo
Msimwa (21).
Kamanda Mallya ametoa wito kwa madereva na
makondakta kufuata sheria za usalama barabarani bila Shuruti pia
aliwataka abiria kujisimamia wenyewe pindi waonapo gari limejaa
wanatakiwa wasipande na sio mpaka wamuone askari ndio watii sheria za
usalama barabarani kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake ili
kupunguza ajali ambazo zinaepukika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...