Na Chalila Kubuda,Michuzi TV


Serikali imesema taasisi za elimu ya juu zinakabiliwa na changamoto zinazotokana na mitaala isiyoendana na soko la ajira

Mitaala hiyo kwa Teknolojia ya saa haiksi hali iliyopo ya kumfanya mhitimu kukabili kwenye soko la ajira ambalo si Tanzania bali ni changamoto ya nchi zinazoendelea

Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Amina Shabani wakati akimwakilisha Waziri wa wizara hiyo katika uzinduzi wa mradi wa mageuzi wa sekta ya Elimu kwa Vyuo Vikuu nchini (HEET) kwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)

Amesema kwa upande wa changamoto zingine kwa vyuo ni miundombinu ya kusomea na kufundishia hususani ile ya kidigitali, uhaba wa wahadhiri wa ngazi mbalimbali, mitaala isiyoendana na uhalisia wa soko la ajira.

" Serikali tumeyaona haya ndiyo maana Serikali ikaja na mradi huu ambao ni matokeo ya mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia katika kwenda kwenye mageuzi ya elimu yanayoendana na mazingira ya sasa," amesema.

Amina ameitaka kamati hiyo kutambua malengo na kazi zake ili iweze kubaini, kushauri na kupendekeza mahitaji na mwelekeo wa mahitaji ya soko la ajira yanayoendana wahitimu kuweza kuyakabili.

"Kwa kufanya hivyo kamati itaweza kuendeleza malengo ya programu na katika hatua hiyo itaisaidia Taasisi kushughulikia mahitaji ya ajira na taaluma kwa ujumla," amesema.

Pia ameitaka TIA kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo ili kuhakikisha inatelekeza Majukumu yake kikamilifu na hatimaye kufikia malengo yaliyokusudiwa.

"Taasisi itoe ushirikiano wa dhati kwa kamati ili kamati iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo na bila kusahau kamati hiyo nayo itoe ushirikiano kwa taasisi ili kwa pamoja waweze kutekeleza malengo yaliyokusudiwa," amesema Naibu Katibu Mkuu Amina

Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) no miongoni mwa taasisi 23 ambazo ziko katika mpango wa HEET kwenye Mageuzi ya Kiuchumi kwa Vyuo Vikuu Nchini (HEET) kupitia Sh27.6 bilioni zilizotengewa

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa William Palangyo amesema tayari baadhi ya mambo katika taasisi hiyo yamefanyika ikiwemo ujenzi wa mabweni mawili katika kampasi ya Mwanza.

"Kupitia fedha za mradi huo tumesaini mkataba wa usimamizi na Mshauri wa ujenzi wa mabweni mawili katika kampasi ya Mwanza na pia tumenunua vifaa vya Tehama kwa ajili ya kufundishia," amesema Palangyo.

Amesema wamegharamia kazi za ushauri wa tathmini ya athari za mazingira za kijamii kwa ajili ya ujenzi wa jengo la taaluma katika kampasi ya Singida.

"Tumefanikiwa kugharamia mafunzo ya kujenga uwezo kwa viongozi wakuu sita wa taasisi nchini Eswatini na kupeleka Watumishi 13 wa kitengo cha Tehama kwenye mafunzo ya usimamizi na usalama," amesema Profesa Palangyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha Wakili Said Chiguma ameshauri kamati hiyo kuweka watu wa uchumi katika kuangalia mazingira kwa pande mbili ambayo ni mahitaji na kipi kiachotakiwa kuzalishwa katika vyuo.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Amina Shaban akizungumza wakati akizindua kamati ya Ushauri ya Mradi wa HEET Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa William Pallangyo  akitoa maelezo kuhusiana kuwepo mafanikio ya mradi wa HEE kwa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wizara ya Fedha Wakili Said Chiguma akitoa maelezo kuhusiana na Bodi inavyoshauri Taasisi ,jijini Dar es Salaam.Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Mradi wa HEET Profesa Mussa Assad akitoa maelezo ya uzalishaji wa wahitimu unaoendana na mazingira ,jijini  Dar es Salaam.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...