Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga akicheza na wananchi wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga umezindua kampeni ya "ONGEA NAO" Kimkoa ambayo imejikita katika utoaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia, mauaji, mmomonyoko wa maadili kwa makundi mbalimbali lengo likiwa ni kushirikiana na jamii kutokomeza uhalifu ikiwa ni pamoja na Ukatili wa Kijinsia.

Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO katika Mkoa wa Shinyanga imezinduliwa leo Ijumaa Desemba 1,2023 wakati wa Uzinduzi wa Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia ukiongozwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali uliofanyika katika shule ya Msingi Buduhe wilayani Kishapu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga amesema Kampeni ya ONGEA NAO inayotekelezwa na mtandao wa polisi wanawake Tanzania (TPF-NET) ilizinduliwa rasmi Jijini Dodoma mwezi Juni, 2023 na leo katika Mkoa wa Shinyanga na kwamba kilele cha Kampeni hiyo ni mwezi Disemba ,2023.

"Jeshi la Polisi tunawataka wanafunzi, wananchi ,wadau kutambua kuwa mnawajibu wa kupaza sauti na kutoa taarifa za uhalifu katika vyombo vya sheria ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii inayozunguuka, kwani jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi",amesema Kamanda Magomi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga akicheza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

"Ni vyema mkatambua kuwa ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa katika jamii na wahanga wakuu ni watoto na wanawake. Hivyo hamna budi kutoa taarifa za ukatili kwa wakati ili wahalifu waweze kukamatwa na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria",ameongeza Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi amesema matendo ya ukatili wa kijinsia ni pamoja na ubakaji, ulawiti vipigo, kutelekeza familia, kutumikisha watoto na kuwazorotesha masomo, lugha za matusi na ndoa za utotoni huku akiyataja madhara ya ukatili wa kijinsia kuwa ni pamoja na vifo, mimba za utotoni, maradhi yanayosababishwa na ngono mfano UKIMWI, ulemavu wa kudumu, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, umaskini, msongo wa mawazo, na migogoro ya kifamilia.


"Pia mnapaswa kutambua mifumo mbalimbali ya utoaji taarifa za ukatili wa kijinsi ambayo ipo katika jamii zetu. Mifumo hiyo ni pamoja na viongozi wa dini, dawati la jinsia polisi, ustawi wa jamii, viongozi wa serikali za mitaa au mtu yeyote anaaminika anaweza kutoa msaada. Hivyo basi niwaombe au nitoe rai kwa wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga tuungane kwa pamoja mkoa wetu uendelee kuwa salama kwenye kampeni hii husuani kwenye masuala mazima ya utoaji elimu kwa wananchi wa rika zote",amesema Kamanda Magomi.

Aidha amesema kesi nyingi za matukio ya ukatili wa kijinsia zimekuwa zikiripotiwa na kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kupelekwa mahakamani na kupata hukumu ambapo kwa sasa kuna mwitikio mkubwa wa kuripoti matukio hali inatokana na elimu inayotolewa na Jeshi la Polisi na ushirikiano mzuri na vyombo vingine vinavyoshughulikia kesi hizi ikiwemo Mahakama, Hospitali, Idara ya ustawi wa jamii, Viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa dini.

Kwa upande wake, Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed ameitaka jamii kutoyafumbia macho matukio ya ukatili wa kijinsia na badala yake kila mmoja awe mstari wa mbele kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia ili jamii iwe salama.
Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja .

Naye, Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja ameishukuru Serikali namna inavyoshirikiana na World Vision Tanzania katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto huku akisisitiza kuwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto unatokomezwa kabisa wilayani Kishapu.

Amesema, katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Mtandao wa Polisi Wanawake wametoa mafunzo ya ukatili wa kijinsia katika jamii zikiwemo shule za Msingi Shiya, Lagana na Sekondari Mwakipoya.

"Sisi World Vision Tanzania tunafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunapinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ili kuhakikisha jambo hilo linatimia kikamilifu, tunazo shughuli mbalimbali tunazozitekeleza katika wilaya ya Kishapu. Miongoni mwa shughuli hizo ni utetezi wa mtoto ambapo tunahakikisha tunaunda na kujengea uwezo kamati mbalimbali kama vile MTAKUWWA, Mabaraza ya watoto na kuhakikisha yanafanya kazi kikamilifu katika kupinga ukatili dhidi ya mtoto na mwanamke",amesema Masanja.
Ugawaji wa mahitaji mbalimbali kwa watu wenye uhitaji katika kaya 50 kata ya Kishapu ukiendelea ambapo wamepatiwa mchele ,sabuni  sukari, maharage na mafuta ya kula.

Ameeleza kuwa pia wana shughuli za maashirio ambapo wanaungana na serikali kuinua uchumi wa kaya ambapo mwanamke ni kipaumbele chao kwa maana kwamba wanapomuinua mwanamke kiuchumi wanakuwa wamejihakikishia kuwa hatanyanyasika tena na changamoto mbalimbali zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia

"Hali kadhalika tunafanya shughuli za afya pamoja na lishe na katika shughuli hizi tunaangazia afya ya mtoto katika umri wa miaka mitano na kuendelea na chini ya miaka mitano. Pia tunatoa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni kwenye maeneo yetu ya miradi na tunaendelea kufanya kampeni kwa wazazi ili programu hiyo iwe endelevu kwamba mtoto anapokuwa shuleni hapati njaa, kupinga unyanyasaji maeneo ya shuleni", ameongeza Masanja kutoka World Vision ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO.


Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia umeenda sanjari na ugawaji wa taulo za kike na madaftari kwa wanafunzi na kutoa mahitaji mbalimbali kwa watu wenye uhitaji katika kaya 50 kata ya Kishapu ambapo wamepatiwa mchele kilo 250, sabuni miche 50, sukari kilo 100, maharage kilo 100 na mafuta ya kula lita 50.
Maadhimisho hayo pia yameambana na burudani mbambali ikiwemo ngoma ya Jeshi la sungusungu, nyimbo, kuvuta kamba, mashindano ya mpira wa pete (Netball) kwa askari Polisi na watumishi wa Halmashauri wilaya ya Kishapu, mashindano ya mpira wa miguu kati ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kishapu na Igaga n.k ambapo washindi wamepatiwa zawadi mbalimbali.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huadhimishwa duniani kote kuanzia tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Disemba kila mwaka kwa lengo la kukuza uelewa wa masuala ya ukatili kwa wananchi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Desemba 1,2023 katika viwanja vya shule ya Msingi Buduhe wilayani Kishapu - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET) Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kishapu (OCD) Esther Zephania Gesogwe akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Msanii Nyumbu Mjanja akitoa burudani ya wimbo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Wadau wakiwemo viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vinavyosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Wilayani Kishapu wakifuatilia matukio wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Mabango mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mabango mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mabango mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mabango mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mabango mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Burudani ikiendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mwanafunzi akitoa burudani ya wimbo
Burudani ikiendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Wanafunzi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya ONGEA NAO na Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia
Mahitaji mbalimbali yaliyotolewa kwa watu wenye uhitaji katika kaya 50 kata ya Kishapu 
Ugawaji wa mahitaji mbalimbali kwa watu wenye uhitaji katika kaya 50 kata ya Kishapu ukiendelea ambapo wamepatiwa mchele ,sabuni  sukari, maharage na mafuta ya kula.
Ugawaji wa mahitaji mbalimbali kwa watu wenye uhitaji katika kaya 50 kata ya Kishapu ukiendelea ambapo wamepatiwa mchele ,sabuni  sukari, maharage na mafuta ya kula.
Ugawaji wa mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi ukiendelea ambapo wanafunzi wamepatiwa taulo za kike na madaftari
Ugawaji wa mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi ukiendelea ambapo wanafunzi wamepatiwa taulo za kike na madaftari
Picha ya kumbukumbu baada ya ugawaji wa mahitaji mbalimbali

Mratibu wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Wilaya ya Kishapu Yohana Masanja (kulia) akimwelezea Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed (aliyevaa kiremba) kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika la World Vision Tanzania katika kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto
Mmoja wa wajasiriamali waliowezeshwa na Shirika la World Vision namna ya kutengeneza vyakula vinanvyotokana na mazao ya lishe na ufugaji nyuki akimonesha bidhaa wanazozalisha Mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed na viongozi mbalimbali
Mashindano ya kuvuta kamba yakiendelea
Mchezo kati ya Kishapu na Igaga ukiendelea
Picha ya kumbukumbu na wachezaji wa timu ya askari polisi
Mchezo kati ya Kishapu DC na Polisi ( waliovaa jezi za bluu) ukiendelea
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akikabidhi zawadi ya mpira kwa timu ya mpira wa pete (Netball) Halmashauri ya Kishapu baada ya kuibuka washindi dhidi ya timu ya Askari polisi

Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu Bi. Fatma Mohamed akikabidhi zawadi ya mpira kwa timu ya mpira wa miguu ya Kishapu baada ya kuibuka washindi dhidi ya timu ya Igaga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...