Ofisa wa Polisi kutoka Makao makuu ya kikosi cha usalama barabarani Tanzania, Mkaguzi msaidizi , Faustina Ndunguru (wapili kulia) akitoa elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji wa barabara na hasa wapanda pikipiki wakati wa kampeni ya Okoa Maisha iliyoandaliwa na ABInBev ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) inayoelimisha madereva kuzingatia alama za barabarani na kuendesha vyombo hivyo kwa kufuata sheria ya usalama barabarani na kuzingatia udereva wa kujihami muda wote wanapotumia barabara, Kampeni hiyo ilifanyika katika eneo la Ubungo kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Sam Nujoma Jijini Dar es salaam. Kulia ni ASP. Mwashamba Onesmo aliyeshiriki katika utoaji elimu hiyo.

Mratibu kutoka StudioRed Communications, Fatma Twalib akiwaelimisha waendeshaji wa vyombo vya usafiri kufuata sheria za barabara wakati wa kampeni ya Okoa Maisha iliyoandaliwa na ABInBev ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL).





Mratibu Mkuu wa kampeni ya Okoa Maisha kutoka StudioRed Communications, Arnold Lazaro akielezea jambo wakati wa kampeni hiyo iliyoandaliwa na ABInBev ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya Bia Tanzania (TBL) inayoelimisha madereva kuzingatia alama za barabarani na kuendesha vyombo hivyo kwa kufuata sheria ya usalama barabarani na kuzingatia udereva wa kujihami muda wote wanapotumia barabara, Kampeni hiyo ilifanyika katika eneo la Ubungo kwenye makutano ya barabara za Morogoro na Sam Nujoma Jijini Dar es salaam.




Watoa huduma ya vibandiko(stickers) wakibandika kwenye vyombo vya usafiri


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...