Wizara imepokea taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ya kuufungia uwanja wa Uhuru kutotumiwa katika michezo inayoendelea ya Ligi Kuu kutokana na kutokidhi vigezo vya kikanuni vya kutumika katika michezo hiyo.

 

Wizara inapenda kufafanua kuwa viwanja vya Uhuru na Benjamin Mkapa vilivyoko jijini Dar es salaam vilitangazwa kuingizwa katika mpango wa ukarabati mkubwa tangu Julai, 2023 ambapo vilipaswa kutokutumika kwa michezo ya Soka ikiwemo Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa.

 

Hata hivyo, kutokana na maombi ya timu zinazocheza Ligi Kuu na uhitaji mkubwa wa viwanja hivyo kwa ajili ya michuano ya Kimataifa, Wizara iliridhia ombi la kuendelea kutumika kwa viwanja hivyo wakati ukarabati ukiendelea.

 

Kazi ya ukarabati mkubwa inaendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Uhuru upo mbioni kuanza baada ya taratibu za kumpata mkandarasi kukamilika.

 

Kwa kuwa ni muhimu kuzingatia kanuni zinazosimamia Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa, Wizara inatangaza kuvifunga viwanja vya Benjamin Mkapa na Uhuru mpaka hapo ukarabati utakapokamilika Oktoba, 2024.

 

Kwa taarifa hii timu zilizoomba kutumia viwanja hivi kama viwanja vyao vya nyumbani zinajulishwa kutafuta viwanja vingine. Wizara inaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao wanamichezo wataupata kutokana na kufungwa kwa viwanja hivi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...