Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro,

Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA mkoa wa Kilimanjaro,imelazimika kutoa kibali kwa mabasi madogo ya abiria maarufu kama Coaster  ya  kukodi "special hire"ili kubeba abiria kuelekea wilaya ya Rombo kutokana na wingi wa abiria kulikopelekea kuwa na uhaba mkubwa wa usafiri kwenye njia  hiyo jumapili iliyopita

Mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi kwa njia zote na kuelekeza mabasi kutoa kibali kwenye  njia zenye uhitaji wa abiria wengi na kuchukua hatua kwa gari za ruti kuzidisha nauli na kuvunja sheria ya usafirishaji 

Akizungumzia adha hiyo Kwa waandishi wa habari Afisa mfawidhi mamlaka ya udhibithi usafiri ardhini LATRA mkoa wa Kilimanjaro Paul Nyello amesema katika kipindi hiki cha sikukuu ya krimasi kuanzi Desemba 23-24 abiria ni wengi na magari kutosheleza mahitaji.

" Tarehe 23 na 24 abiria walizidi kushinda uwezo wa mabasi ya njia za Rombo na Tarakea ambapo ndipo kuna abiria wengi zaidi Mamlaka imechukua hatua kwa kuchukua magari makubwa kama coaster za kukodi maarufu special hire  na kupatana bei nafuu kwa abiria ,"amesema Nyello 

"Mabasi makubwa ya masafa marefu kama Ngasere alitoa huduma ,"

Amesema kuwa magari ya kukodi special hire yalituka kuwabeba abiria katika njia hiyo kwa bei ya kupatania kwani yale magari yanasheria zake na utaratibu kutokana na yapo kwa ajili ya kukodiwa.

Amesema mamlaka ikishirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani walikuwa stendi na kuhakikisha abiria wote wanapata usafiri.

Amesema kuwa mamlaka hiyo pia ilifanya ukaguzi kwenye magari yote ya ruti za ndani na kuhoji abiria kama wamezidishiwa nauli lakini hakukuwa na abiria yoyote aliyelalamika.

Natoa wito kwa baadhi ya waandishi wa habari kuhakiki taarifa toka Mamlaka kupata ufafanuzi wa kina kwa kuwa wakati mwingine wanaotoa taarifa potofu kwa kutojua nini kinafanyika na Mamlaka na wao kuchukua taarifa upande  mmoja.

Nao baadhi ya abiria wakizungumza kwa nyakati tofauti na wandishi wa habari wameshukuru LATRA kwa kusimamia vema suala la nauli kuwasaidia kuwapatia usafiri kutokana magari katika njia Rombo Tarakea kutosheleza mahitaji yote ya abaria.

Abiria Amalia Shirima amesema kuwa usafiri wa Rombo ulikuwa shida lakini kulikuwepo watu LATRA ambao walituletea magari yale yakukondiwa,kweli tunawashukuru walihakikisha tunasafiri salama.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...