Na Munir Shemweta, WANMM MLELE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesheherekea Siku Kuu ya Chrismas akiwa katika jimbo lake la Kavuu lililopo wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Akiwa jomboni humo, Naibu Waziri Pinda alishiriki ibada ya Chrismas katika Kanisa Katoliki Parokia Teule ya Bikira Malia Mpalizwa Mbinguni Kibaoni ambako alishiriki pia harambee ya ya ujenzi wa Nyumba za Mapadri wa Kanisa hilo na kuahidi kuchangia mifuko 200 ya Saruji. Ujenzi wa nyumba hizo utagharimu shilingi milioni 75.

Ibada hiyo ya Chrismas katika kanisa hilo ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda.

Aidha. Naibu Waziri Pinda akiwa eneo la Kibaoni ambapo ndipo yalipo makazi yake wilayani Mlele mkoani Katavi alijumuika na baadhi ya wananchi wa eneo hilo wakiwemo viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mlele katika kusheherekea siku hiyo ya Noeli.

Naibu Waziri Pinda yuko jimboni kwake katika jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi pamoja na mambo mengine kujumuika na wapiga kura wake kutafakari utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika jimbo hilo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda akizungumza na baadhi ya wananchi waliomtembelea nyumbani kwake Kibaoni katika jimbo la Kavuu tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mlele Wolfgun Pinda (Katikati) akiwa jimboni kwake tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda (katikati) akizungumza na mmoja wa wananchi wa Kibaoni, Mlele wakati akiwa jimboni kwake tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mlele Wolfgun Pinda.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu wilayani Mlele mkoa wa Katavi Mhe Geophrey Pinda akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofika nyumbani kwake Kibaoni, Mlele akiwa jimboni kwake tarehe 25 Disemba 2023 mkoani Katavi.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...