NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.


KIONGOZI Mkuu wa Matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Machano Ali Machano ,amewasihi Maafisa Usafirishaji(bodaboda) wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kuwa makini wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ili kupunguza ajali.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na kusikiliza changamoto za bodaboda katika Matembezi hayo Pemba.


Machano,alisema umakini ndio nyenzo pekee ya kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi kwa ufanisi.


Alisema kuwa UVCCM ina dhamana kubwa ya kuyasemea makundi mbalimbali ya vijana ili changamoto zao zitafutiwe ufumbuzi na taasisi husika.

Katika mKEEaelezo yake,Mkuu huyo wa Matembezi alisema Serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi,inaendelea kutoa fursa za mikopo yenye masharti nafuu hivyo kundi hilo wafuate utaratibu na UVCCM itawasemea kuhakikisha wananufaika na mikopo hiyo.


“Matembezi ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ni jukwaa la kutuunganisha vijana wa makundi mbalimbali kukaa pamoja na kujadiliana kwa kina mafanikio na changamoto mbalimbali zinazotukabili ili kupata namna bora ya kuzitatua


”UVCCM tutaendelea kuwasemea mema pamoja na kuhakikisha asilimia za fedha zinazotengwa na Serikali kwa ajili ya uwezeshaji wa kundi la vijana kutoka Mabaraza ya Manispaa na Halmashauri zinawanufaisha nyinyi katika kupata mitaji na kujikwamua kiuchumi,alisema Machano.

Machano, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki amelitaka kundi hilo la Maafisa usafirishaji kujiepusha na vitendo vya matumizi ya dawa za kulevya,udhalilishaji wa kijinsia na ukabaji badala yake waendelee kuwa waaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohamed Ali Kawaida,alisema aliwapongeza Maafisa usafirishaji hao kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutoa huduma za usafiri kwa wananchi wa makundi mbalimbali.

Kupitia kikao hicho Mkuu huyo wa Matembezi Machano Ali na Mwenyekiti wa UVCCM taifa Mohamed Kawaida pamoja na Viongozi mbalimbali wa UVCCM wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,waligawa mavazi maalum ya kuwasadia kutambulika kwa urahisi wakati wa utendaji wa kazi zao hasa usiku(Reflectors)kwa Maafisa wote wa Usafirishaji.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...