Chama cha Waandishi waendesha ofisi (TAPSEA), Mkoa wa Dodoma kimetoa pole na msaada wa vifaa mbalimbali kwa waathirika wa maporomoko ya tope yaliyotokea Wilayani Hanang Mkoani Manyara.

msaada huo ambao ni mchango wa TAPSEA mkoa wa Dodoma ni pamoja na vifaa vya shule yakiwemo madaftari, sare za shule, kalamu na nguo vyote vikiwa na jumla ya takribani shilingi milioni 5.

Mwakilishi wa Chama hicho Bi, Conjeta Chambila amesema chama chao kimeona umuhimu wa kuchangiana kwa lengo la kuweza kuwasaidia wenzao.

Pia Bi Chambila, amemshukuru Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi Balozi, Mhandisi Aisha Amour kwa kuweza kuwawezesha usafiri wa kutoka Dodoma hadi kufika Mkoani Manyara.

“ Tunamshukuru sana Katibu Mkuu wa ujenzi, kwa kuweza kutukusanya pamoja na kutuwezesha kutupa usafiri, ikiwa tunatoka Ofisi mbalimbali” amesema Chambila.

Aidha, Chama hicho kimetoa wito kwa waandishi waendesha ofisi wengine wa mikoa ya karibu kuweza kuwasaidia waathirika hao ambao wamepoteza vitu vyao wakati wa maafa hayo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala ( DAS), Mkoa wa Manyara, Bw. Athuman Likeyekeye amewashukuru Waandishi waendesha Ofisi kutoka mkoa wa Dodoma kwa upendo wao wa kuja kuwasaidia waathirika hao katika kipindi hiki cha Sikukuu za Mwaka mpya.

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na uratibu, kwa kushirikiana na ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya, wanaendelea kupokea misaada mbalimbali kwa ajili ya waathirika wa maporomoko ya tope, Mkoani Manyara. 





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...