Na Brown Jonas - WUSM

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili kuhusu tukio la mbio za pamoja za kudumisha ushirikiano kati ya Tanzania na India "The Friendship Run between India and Tanzania with Milind Soman" linalotarajia kufanyika jijini Dar es salaam kati ya tarehe 30 na 31 Desemba,2023.

Akizungumza kuhusu tukio hilo leo Desemba 5,2023 Mhe. Ndumbaro amesema Serikali ya India imeomba ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kufanikisha tukio hilo ambalo pia litahudhuriwa na mwanariadha maarufu kutoka nchini India Milind Soman.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...