
Na Karama Kenyuko, Michuzi Tv
UONGOZI WLwa Benki ya Mwalimu (MCB), umezindua kampeni ya Kapu la MwalimuSanta ili kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kugawa zawadi mbalimbali kwa wateja wake.
Miongoni mwa bidhaa zilizomo ndani ya Kapu la MwalimuSanta ni fao la wastaafu watarajiwa na waliostaafu tayari, bima ya nyumba ama samani za ndani na zawadi za sh. 50,000 kwa wateja watano kila wiki watakaotoa fedha kwa wakala bila kadi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kapu la MwalimuSanta, Meneja Masoko wa MCB, Hannah Mbajo amesema uongozi wa benki hiyo umedhamiria kurudisha shukrani kwa wateja wake.
Mbajo alisema Kapu la MwalimuSanta limebeba bidhaa muhimu kwa wastaafu watarajiwa na waliostaafu tayari ambao watawekeza fedha zao kwa faida ya asilimia 12 kwa mwaka na kupata bila malipo bima ya nyumba na samani za ndani.
"Wastaafu wengi wanakwama kwenye biashara sababu hawana uzoefu, sisi MCB tumekuja na suluhu ya mafao yao ya kustaafu. Watuamini tuwawekee fedha hizo wakiwa na uhakika wa kupata faida kila mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka.
"...Kapu la MwalimuSanta halikuishia hapo likaendelea kwa kuwalipia wastaafu bima ya nyumba kama anayo ama samani zote za ndani.
"Sote tunaona hivi sasa majanga mbalimbali yameongezeka kuna moto, mafuriko kama kule Manyara na hii ni kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi hivyo tunamkinga mstaafu wetu na majanga ya aina yoyote," alisema Mbajo.
Akifafanua zaidi Mbajo alisema MCB ni sehemu salama kabisa kuwekeza kwa wastaafu ambao wanaweza kuchukua fedha zao wakati wowote huku wakijihakikishia usalama wa mali zao kwa kupatiwa bima.
Alisema Kapu la MwalimuSanta linamruhusu mstaafu aliyewekeza fedha zake MCB kukopa asilimia 80 ya fedha alizowekeza kupitia mkopo wa 'Mlinde Mstaafu'.
Akizungumzia bidhaa nyingine iliyopo kwenye Kapu la MwalimuSanta, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidigitali cha MCB, Elilumba Kinyau alisema kapu hilo pia linagawa zawadi hadi sh. 50,000 kwa wateja wake watakaofanya muamala wa kiwango chochote bila kadi kupitia kwa wakala.
"Hii ni zawadi kwa wateja wetu watano kila wiki kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka mteja akitoa hela bila kadi kwa wakala wa MCB popote alipo atajipatia fedha taslim hadi sh 50,000 hapohapo," alisema Kinyau.
Alisema MCB ina mawakala zaidi ya 500 nchi nzima na huduma za benki kiganjani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...