Na Mwandishi wetu,Jeshi la Polisi-Dodoma.

Jeshi la Polisi nchini limesema  kuwa litawafungia leseni madereva wote wanaosababisha ajali huku likibainisha  kuwa katika siku za hivi karibuni kumeendelea kujitokeza ajali za barabarani zilizosababisha vifo na majeruhi kwa watanzania ambapo. Chunguzi zinapofanyika zinaonyesha chanzo ni uzembe wa madereva wanaoendesha magari hayo.

Akitoa taarifa hiyo leo disemba 06,2023 msemaji wa Jeshi la Polisi nchini  kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime  amesema kuwa chanzo cha ajali hizo ni  Uzembe pamoja na mwendo kasi na kupita magari mengine (overtake) bila kuchukua tahadhari maeneo ambayo alama za barabarani zimekataza.

Ameendelea kusema kuwa pamoja na uzembe huo unaofanywa na baadhi ya madereva, wa magari hayo kumekuwa na maneno ya kuiaminisha jamii kuwa mwisho wa mwaka ajali zinakuwa nyingi, jambo ambalo si sahihi huku akiwataka madereva kuondoa dhana hiyo ambayo inapotosha umma wa Tanzania.

SACP Misime amebainisha kuwa kufika kwa mwisho wa mwaka hakujabadili sheria za usalama barabarani wala alama za makatazo na ishara za barabarani.ambapo amewataka madereva kuzifuata sheria hizo ili kuepuka ajali za barabarani.

Aidha Msemaji wa Jeshi hilo amewambia madereva na wananchi kuwa  kinachobadilika ni tabia za baadhi ya madereva wa vyombo vya moto wasiotaka kuzingatia sheria za usalama barabarani na kufuata alama za makatazo na zile za ishara za barabarani na matokeo yake wanasababisha ajali.

Sambamba na hilo amesema Jeshi la Polisi nchini linapenda kusisitiza, kuwa kwa watumiaji wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu, wasukuma mikokoteni, waendesha baiskeli na waendesha vyombo vya moto wazingatie sheria za usalama barabarani huku akiwaomba Viongozi wa serikali kuwaonya madereva wao pale wanapokiuka sheria za usalama barabarani.

Msemaji wa Jeshi hilo amewambia waandishi wa Habari kuwa Jeshi la Polisi nchini litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kuwafutaia leseni zao ikiwa ni Pamoja na kuwafikisha mahakamani kwa makosa hayo ya usalama barabarani.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...