Na Fauzia Mussa, MAELEZO
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto RIZIKI PEMBE JUMA amesema Serikali kupitia Wizara hiyo imeandaa mikakati maalumu ya kuwawezesha Wanawake wajane waliotelekezwa na Watoto.
Akizungumza na Rais wa Umoja wajane wa Afrika na Ujumbe wake huko Ofisini kwake Mhe. Riziki amesema hatua hiyo inasaidia kuwaandaa kisaikolojia na kuweza kukabiliana na maisha baada ya tukio hilo.
Aidha alifahamisha kuwa Wizara yake imekuwa ikitoa ujuzi wa ujasiria Mali pamoja na kutoa mikopo midogomidogo kwa akina mama hao ili kuanzisha biashara itakayosaidia kumudu gharama za maisha ya mama na mtoto.
Nae raisi wa wajane wa Afrika Hope Nwakwesi alisema ipo haja ya jamii kupatiwa elimu juu ya madhara yatokanayo na talaka kwani hali hiyo imekuea ikipelekea kwa kiasi kikubwa kupoteza nguvukazi ya Taifa , kukosa jamii yenye upendo na kuwa na watoto wasio na muoelekeo mzuri wa misingi ya maisha kwa kukosa malezi ya baba na mama.
Daktari wa Magonjwa ya Afya Aya akili Zanzibar Dkt. Khadija Abdulrahman Omar alisema wajane wengi hufikiria juu ya namna gani wataweza kumudu gharama hizo binafsi na kwa watoto wao jambo linalopelekea kuathirika kisaikolojia na kupelekea kuugua ugonjwa wa Afya ya akili.
"Takwimu zinaonesha nusu ya wagonjwa Wanawake wanaolazwa kwa ugonjwa waafya ya akili inasababishwa na ujane iwe wa kuachwa au kuondokewa na mwenza ."alifahamisha Dkt Khadiaja
Hata hivyo alisema Serikali inaendelea na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na Ongezeko la wagonjwa wa Afya ya akili na kuiomba Ofisi ya mufti kuyafanya Mafunzo ya kuwajengea uelewa kabla ya ndoa kuwa ni ya lazima wakihusisha wataalamu wa Afya yaakili katika mafunzo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi TAASISI ya wajane Tanzania Rose sarot amesema wajane wamekuwa wakipunguza nguvu kazi na upendo kwa familia kadiri wanavyoendelea kukaa hospitalini wakiugua ugonjwa wa Afya ya akili.
Alifahamisha kuwa Maamuzi ya talaka hayamuathiri Mjane peke yake Bali huathiri hata watoto na kuwataka wanandoa na wenza kufikiria muelekeo wa watoto kabla ya kutengana au kupeana talaka kwani nao ni miongoni mwa waathirika wakubwa baada ya tukio hilo .
" tunapofukia hatua ya Kua tumechokana tuangalie na watoto tuangalie nguvu kazi inayopotea kwa kuugua muda mrefu wewe upo hospitali watoto wapo sehemu Fulani wanadhalilika na kuteseka,mwisho nao wataugua magonjwa ya akili"alifahamisha bi Rose.
Alifahamisha kuwa migogoro kati ya wawili hao sambamba na kufariki kwa Baba huchangia kumpa mtoto msongo wa mawazo na hatimae kuugua Afya ya akili.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Wajane Zanzibar Tabia Makeme amesema ipo haja ya kushirikiana kwa pamoja kati ya Taisisi zinashughulikia maswala hayo ,kituo cha Afya ya akili na Ofisi ya Mufti ili kupunguza ongezeko la wajane linalopelekea wimbi la wagonjwa wanawake wanaogua Afya ya akili.
Amesema hali ya magonjwa ya akili kwa wajane sio nzuri na jumuiya hizo haziridhishwi na hali hiyo hivyo aliishauri jamii kutokuingia katika ndoa bila ya kuwa na elimu nzuri itakayowawezesha wawili hao kuweza kuvumiliana na kupelekea kupeana talaka.
Katika ziara hiyo ya siku moja Umoja wa wajane Afrika ulipta fursa ya kutembelea Hospital ya magonjwa ya akili Kidongo Chekundu ,Tume ya Ukimwi na Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto kuelekea mkutano mkuu wa siku ya wajane Duniani unaotarajiwa Kufanyika Mwakani Visiswani Zanzibar.
Ujumbe wa Taasisi za wajane Afrika wakipiga ngoma walipotembelea kitengo cha tiba kwa vitendo kwa watu wenye ugonjwa wa akili wakati walipotembelea Kituo hicho huko Kidongo Chekundu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...