NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOSHI
MADAKTARI
wenye ujuzi wa kufanya tathmini ya ulemavu unaotokana na ajali na magonjwa
yatokanayo na kazi (Impairment Assessment of Occupational Accidents and
Diseases) wamefikia 1,722 Nchi nzima, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin
Babu, amesema.
Mhe.
Babu amesema hayo mjini Moshi, Desemba 5, 2023, wakati akifungua mafunzo ya
ya kuwajengea uelewa madaktari na watoa huduma za afya, kufanya tathmini ya ulemavu unaotokana na ajali na
magonjwa yatokanayo na kazi (Impairment Assessment of Occupational Accidents
and Diseases).
“Ili
Mfuko uweze kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha wafanyakazi wanaopata
ulemavu au magonjwa yatokanayo na kazi, wanapata fidia stahiki na kwa wakati,
lazima wawepo madaktari wenye ujuzi wa kufanya kazi hiyo.” Amefafanua.
Alisema
WCF, ambayo ilianza kutekeleza majukumu yake miaka 8 iliyopita, ilianza zoezi
hili la kutoa mafunzo katika mwaka wa fedha 2015/16 mpaka sasa.
“WCF
inatuhakikishia kuwa itaendelea kutoa mafunzo haya kwa wadau wengi zaidi ili
kuweza kutimiza nia njema ya Serikali iliyopelekea kuundwa kwa taasisi hii
muhimu.” Amesema Mhe. Babu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma amebainisha kuwa, mafunzo
hayo yamewaleta pamoja madaktari 100 kutoka hospitali za umma na binafsi, kwa
ngazi zote, kuanzia vituo vya afya hadi hospitali za rufaa za kanda.
“Awali
uelimishaji wa aina hii ulianzia ngazi ya hospitali za Wilaya, hata hivyo, ili kuhakikisha Mfuko
unaendana na kasi ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, ya kufungua Nchi, ambapo uwekezaji umeongezeka katika maeneo
mbalimbali, na si tumeona tupanue wigo wa kuelimisha wataalamu wetu kuanzia
ngazi ya vituo vya afya.” Amefafanua Dkt. Mduma na kuongeza..hii itasaidia
kusogeza huduma karibu zaidi kwa walengwa,” amefafanua.
Akizungumzia
mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, amesema,
baadhi ya mambo ambayo madaktari hao wamejifunza ni pamoja na Sheria ya Fidia
kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015], Mchakato wa Uwasilishaji
Madai, Dhana ya Usalama na Afya mahali pa Kazi, Jinsi ya Kudhibiti Vihatarishi
sehemu za kazi, Jinsi ya kufanya Tathmini ya Vihatarishi, Kuchunguza magonjwa
yatokanayo na kazi, Udhibiti wa Ajali na Magonjwa mahali pa kazi, jinsi ya
kufanya Tathmini ya Ulemavu, Jinsi ya kufanya Tathmini ya Magonjwa yatokanayo
na kazi na Mafao yatolewayo na Mfuko
Wakitoa
maoni yao kuhusu mafunzo hayo, baadhi ya washiriki walisema, yamewajengea
uelewa mzuri wa namna ya kumuhudumia mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na
kazi lakini pia kutambua kuwa hata wao pia huduma za WCF zinawahusu.
Dkt.
Cresencia Edmond, kutoka Hospitali ya St. Elizabeth, amesema, amefurahi kupata
ujuzi mpya kuhusiana na kazi zake lakini hata yeye binafsi kama mfanyakazi.
“Elimu
ya kujiepusha na vihatarishi vinavyoweza kupelekea mtu kuathirika na magonjwa
au ajali zitokanazo na kazi, mfano maumivu ya mgongo (back pain)
yanayosababishwa na ukaaji au matumizi ya viti visivyofaa kiafya.” Amesema Dkt.
Edmond.
Naye
Dkt. AzariaSimon mshiriki kutoka hospitali ya Haidom, yeye amesema
amefurahishwa na Dhima (Mission) ya Mfuko ambayo ni kupunguza athari za kijamii
na kiuchumi za majanga yatokanayo na kazi kwa wafanyakazi, familia zao na
waajiri kwa kutoa fidia stahiki, kwa usawa, uendelevu na ufanisi.
“Hiyo
ndiyo nimeipendelea pamoja na mambo mengine kama vile jinsi ya kutoa taarifa
kupitia mifumo, mtu (mfanyakazi) anapopatwa na matatizo akiwa kazini.” Amefafanu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...