Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko, ameungana na wasanii wa filamu zaidi ya 50 wa mkoa wa Dar Es Salaam katika Pori la Akiba Pande ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuendelea kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii.

Katika ziara yake aliongozana na Kamanda wa Uhifadhi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Sylivester Mushy pamoja na Mkuu wa Uhifadhi Pori la Akiba Pande Dorothy Masawe.

Akizungumza na wasanii hao mara baada ya kupata fursa ya kutembea na kuangalia wanyamapori hai mwenyekiti wa Bodi ya TAWA amewashukuru kwa kitendo chao cha uzalendo katika kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza utalii wa ndani.

Aidha Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko amesema tunategemea kubadilisha jina la eneo hili kutoka Pande Game Reserve na kupata jina zuri ambalo linaweza kuwa icon ya jiji la Dar es salaam, hii yote ni kutokana na nia thabiti ambayo Watanzania mbalimbali wameonesha kufurahia uwepo wa shamba hili la wanyamapori hai, 

“kuja kwenu kumefunua macho ya wananchi wengi kufahamu uwepo wa eneo hili” basi niombe mpate nafasi ya kutembelea Magofu ya Kilwa na kuweza kutengeneza filamu moja ambayo maudhui yake yatajikita katika kutangaza vivutio vyetu mbalimbali vya utalii vinavyoptikana TAWA.

Kwa upande wa wasanii wakiongozwa na mwenyekiti wa mkoa wa Dar Es Salaam Mwinuka, wameushuru kwa mapokezi mazuri na kupata fursa ya kutembea na kuangalia wanyamapori hai kama vile Bundamia, Swala Pala, Nyumbu, Swala Granti na ndege wengi wa aina tofauti waliopo katika Bustani ya wanyamapori ya Pande.

Tukio la kuwaalika wasanii wa filamu zaidi ya 50 akiwepo Mzee Chilo, Dude, Asha Boko, Amina Makabila, Madebe Lidai, Kelvin, Big Matovorwa, Boss Kimaro na Mama Mawigi ambaye muigizaji maarufu Kwa lugha ya Kihaya 

liliandaliwa na Menejimenti ya Pori la Akiba Pande likiongozwa na Kamanda wa Uhifadhi wa Pori la akiba Pande Dorothy Masawe kupitia Kanda Maalum ya Dar es Salaam  chini ya Uongozi wa Kamanda wa Uhifadhi Sylivester Mushy.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...