TAMWA Zanzibar imeiomba jamii kupunguza malalamiko ya udhalilishaji katika Jamii inahitaji kutafuta mbinu za kupambana na vitendo vya udhalilishaji ambavyo vinaripotiwa kuongezeka kiasi cha kuwa na matukio zaidi ya 150 kwa mwezi mmoja tu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, inaonesha kuwa ndani ya mwezi Oktoba matukio yalikuwa ni 199 na mwezi wa Novemba jumla ya matukio 172 yameripotiwa, na katika matukio yote haya waathirika wakubwa wa vitendo hivi ni wanawake na watoto.

katika taarifa ya kufunga mwaka iliyotolewa leo, Desemba 31, 2023 na Mkurugenzi wa Tamwa Zanzibar, Dkt,. Mzuri Issa imesema kuwa ikilinganishwa na idadi ya matukio ya mwaka 2022 anbapo jumla ya matukio 1361 yaliripotiwa, idadi hiyo inaweza kuongezeka kupita kiasi kutokana na idadi kubwa inayoripotiwa kwa kila mwezi ndani ya mwaka 2023.

Imesema Ongezeko hilo linahitaji kuangaliwa katika pande kuu mbili ambazo ni vyombo vya kisheria pamoja na jamii kwamba kwa kiasi gani sehemu hizo zinachukua jukumu lake ipasavyo.

Kwa mfano upande wa vyombo vya sheria vihakikishe haki inapatikana kwa watu wote kama inavyostahiki na kwamba wahalifu wote bila ya ubaguzi walipie makosa yao.

 Pia sheria zinahitaji ziwe vizuri, zinatekelezeka ipasavyo na kwamba Maafisa wa vyombo vya sheria wanashughulikiwa ipasavyo pale wanapokengeuka majukumu yao.

Jamii kwa upande wake inapaswa kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na kutoa elimu kwa watu walioko katika makundi hatarishi ili wasifanye vitendo vya kudhalilisha wengine, kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji na kutoa ushahidi pale inapohitajika.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Mtakwimu kwa mwezi wa Novemba kati ya matukio 172 ni tukio moja tu ndilo lililofikishwa mahakamani hali ambayo inahitaji kuangaliwa vizuri.

Changamoto nyengine ni juu ya ukosefu wa utumiaji mzuri wa sheria kwa mfano sheria ya ushahidi No. 9 ya mwaka: a 2016 imetoa fursa ya kutumia ushahidi wa kielektroniki lakini bado hautumiki ipaswavyo na hivyo kuhatarisha kupotea kwa mafaili na kuleta usumbufu kwa watoa ushahidi hasa watoto na watu wenye ulemavu.

Hivyo, tunatoa wito kwa vyombo vya sheria kuzidisha kasi ya upelelelezi na kuwekeza katika teknolojia kwa ajili ya kusikiliza malalamiko na kuwapa unafuuu watoto wadogo.

TAMWA ZNZ pia inaendelea kutoa wito kwa vijana kujipangia mipango madhubuti ya kutokuingia katika vitendo hivi ikiwemo kuacha kufuata vishawishi, kutokuendekeza mihemuko na pia kujidhibiti dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...