Mshindi wa pesa taslimu shilingi milioni 10 kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, Bi. Juliana Lukwaro (katikati) akiwa ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) na kusindikizwa na msanii wa Bongo Flava, Dogo Janja (kwa nyuma mwenye rasta) na George Venanty, Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini (kwa nyuma mwenye miwani) katika viwanja vya Stendi Kuu mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.
Meneja wa Vodacom Tanzania PLC Kanda ya Kaskazini, Bw. George Venanty, (kulia) akikabidhi mfano wa kadi ya bima ya afya kwa mmojawapo wa akina mama (katikati) na Mganga Mfawidhi Dkt. Edna-Joy Munisi (kushoto), katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kilimanjaro - Mawenzi mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, kampuni hii imekabidhi kadi za bima kwa akina mama 100 na watoto 100 hospitalini hapo ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu.
Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) kutoka Vodacom Tanzania akifurahi pamoja na mmojawapo wa akina mama waliopatiwa bima ya bure kwa mwaka mzima katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kilimanjaro - Mawenzi mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, kampuni hii imekabidhi kadi za bima kwa akina mama 100 na watoto 100 hospitalini hapo ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu.

Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) kutoka Vodacom Tanzania PLC akikabidhi luninga kwa mshindi wa kampeni inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, akishuhudiwa na George Venanty, Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini (kulia) katika viwanja vya Stendi Kuu mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...