Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
RAIS Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Amani Abeid Karume amewataka wahitimu wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS kuitumia elimu waliyoipata kwa kuwatumikia wananchi kwa weredi na upendo huku wakiendelea kujiendeleza zaidi na elimu.

Karume amesema hayo leo Desemba 2, 2023 jijini Dar es salaam katika Mahafali ya 17 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Akizungumza kabla ya kuanza kuwatunuku wahitimu hao stashahada na shahada mbali mbali chuoni hapo Karume amesema, ili wahitimu hao waweze kuisaidia jamii na Taifa zima kwa ajili ya kuiletea nchi yetu maendeleo basi wanapaswa kujitolea kufanyakazi kwa upendo mkubwa.

"Huu sio mwisho, leo mnatunikiwa ili muende mkaisaidie jamii yenu kwa upendo kwani upendo ndio maendeleo ya elimu katika taifa na pia wengine muendelee kujiendeleza kielemu zaidi"amesema Karume.

Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema wataendelea kutoa elimu kuendena na teknolojia na kufanya tafiti ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya afya.

Pia ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa michango yao iliyokowezesha chuo kutekeleza majukumu yake katika nyanja za ufundishaji, tafiti na huduma kwa jamii.

Aidha prof Kamuhabwa ameipongeza serikali kwa kuongeza rasilimali watu katika chuo hicho ambapo takribani wanataaluma 111 na wasaidizi wa taaluma 11 wameajiliwa chuoni hapo.

"Tutaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha idadi ya watumishi inaongezeka kulingana na uhitaji unaohitajika lakini pia chuo kimeshirikiana na serikali kuboresha miundombinu ya chuo lakini kuendelea kushirikiana ili tufanikishe ujenzi wa chuo kipya Kigoma"amesema Kamuhabwa.

Nae,mwakilishi wa wahitimu wa shahada za awali Whitefrank Frank,ambae ni muhitimu wa shahada ya udaktari wa kinywa na meno amesema ni wajibu wao kubeba majukumu waliyopewa kwa nidhamu,weredi na upendo kwani wameichagua fani ya afya wao hivyo awanabudi kuitumikia.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa wahitimu wa shahada za uzamili Merciana Mliga amepongeza jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya afya kwa kuweka mazingira wezeshi ya ufanyajikazi lakini ufadhiri wa masomo kwa ngazi mbalimbali.

"Shukrani za pekee ziende kwa serikali ya jamuhuri ya muungano inayoongozwa na mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan amejitoa kwa nguvu zote katika kuboresha sekta ya Afya na elimu kwa kuweka miundombinu wezeshi ya kujifunzia na kufanyia kazi"amesema Mliga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...