Na; Mwandishi Wetu - Bujumbura, BURUNDI
Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameendelea kuthamini mchango unaotolewa na sekta isiyo rasmi katika kuleta maendeleo ya nchi hizo ikiwamo kukuza ajira.


“Lengo la kuanzisha maonesho hayo lilikuwa ni kuwapatia fursa wajasiriamali ili waweze kushiriki kwa wingi katika shughuli za uzalishaji na kuwawezesha kukua zaidi” amesema Brig. Jen. Mnumbe
Vile vile, amewataka kuongeza bidii katika kuzalisha bidhaa bora kwa viwango vya kimataifa na kuzitangaza bidhaa hizo ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuongeza wigo wa soko na kuwasihi kushirikiana, kubadilishana ujuzi na masoko katika uzalishaji wa bidhaa na utengenezaji wa vifungashio na kuthaminisha.
Kadhalika, amepongeza wajasiriamali kutoka Tanzania kwa kuandaa bidhaa zenye ubunifu, ubora wa hali ya juu na zenye asili ya kitanzania.
Maonesho hayo ya 23 yamewashirikisha wajasiriamali 1,500 kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiwemo 259 kutoka Tanzania yanafanyika kwa mara ya tatu nchini Burundi tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...