WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa ameagiza wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji kote nchini kutojihusisha na mauzo ya viwanja na vipande vya ardhi.

Aidha ameweka wazi kuwa watakaohusika ni maofisa ardhi kwa kushirikiana na kampuni za upangaji na upimaji wa ardhi kwenye maeneo na miji husika huku akipiga marufuku wananchi kutonunua maeneo ya ardhi ambayo hayajapimwa au kupangwa na Serikali.

Waziri Silaa ameyasema hayo leo Desemba  22,2023 alipokuwa akitoa  tathmini ya siku 100 za utekelezaji tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa Waziri mwenye dhamana na masuala ya ardhi kupitia mkutano wajukwaa la wahariri uliofanyika jijini Dar es Salaam.

"Kwa wale wanaokwenda kununua viwanja vijijini hakikisha umeitishwa mkutano wa kijiji kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa uamuzi wa kupewa ardhi na ikiwezekana tumia simu kurekodi kwa kukubaliwa kupewa hilo eneo," amesema Silaa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...