Na Takdir Ali – Habari Maelezo.
WAZIRI wa Uchumi wa buluu na Uvuvi Suleiman Massoud Makame amesema miradi ya maendeleo imeongozeka katika wizara hiyo kutoka miradi 10 ya maendeleo mwaka 2020 hadi kufikia 17 mwaka 2023.

Ameyasema hayo wakati alipokuwa akilezea makakati na mafanikio ya Wizara hiyo, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema miradi hiyo imejumuisha sekta mbalimbali ikiwemo Uvuvi, Mwani, Ufugaji, Viwanda vya kusarifu madagaa na mwani, masoko na madiko, uhifadhi wa Bahari na utafiti.

Ameeleza kuwa mafanikio hayo ya kimaendeleo yanaifffiisha Serikali katika shabaha za kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050, na Mpango wa Maendeleo ya Zanzibar (ZADEP).

Aidha amesema Serikali inaendelea kuwawezesha wajasiriamali kwa kuwapatia elimu, ubunifu na zana za kujiongezea ajira katika maeneo yao.

Amefahamisha kuwa Serikali imeweka mkakati wa kuwawezesha wakulima wa mwani na wafugaji wa mazao ya baharini 23,000 ambao zaidi ya asilimia 90 ni wanawake wa vijijini.

Mbali na hayo amesema, Usafirishaji wa mwani nje ya Nchi umeongezeka kutoka Tani 11,382 zenye thamani ya Tzs Bilioni 11.70 mwaka 2020 hadi kufikia Tani 12,563 zenye thamani ya Tzs Bilioni 12.581 kwa mwaka 2023.

Sambamba na hayo amesema maendeleo ya kiuchumi na kijamii ni lazima yazingatie uhifadhi wa maliasili hivyo amewaomba Wananchi kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kuleteleza mikakati iliojipangia.

Mbali na hayo amesema Serikali imetilia mkazo utafiti na sayansi ya bahari ili kupata taarifa sahihi zinazoimarisha utekelezaji wa sera za Uchumi wa Buluu.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleimana masoud Makame akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara yake kuelekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi Salum Vuai akiuliza maswali katika Mkutano na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleimana masoud Makame alipokua akizungumzia kuhusiana na Mafanikio na Changamoto za Wizara yake kuelekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...