Na Mwandishi Wetu, Ivory Coast

Wakati mataifa mbalimbali yakiwasili nchini Ivory Coast kwa ajili ya makala ya 34 ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON), timu ya taifa ya Cameroon huenda ikamkosa Nahodha wake, Vincent Aboubakar kwa sababu ya kupata majeruhi akiwa mazoezini wakati wakijiandaa na mashindano hayo.

Taarifa kutoka mitandao mbalimbali zimeripoti kuwa Cameroon (Indomitable Lions) wana mpango wa kutafuta mbadala wa Nahodha huyo ambaye anacheza Klabu ya Besiktas ya Uturuki.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Coton Sport ya nyumbani kwao Cameroon, tangu kuanza kucheza timu hiyo ya taifa, mwaka 2010, amecheza michezo 100, ambapo amecheza Michuano hiyo ya AFCON mwaka 2015, 2017 na 2021 na Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, 2014 na 2022.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...