Na Mwandishi Wetu, Same 

MBUNGE  Wa jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro Anne kilango Malecela amechangia Sh. milioni 20, kwa ajili ya ujenzi   wa Shule ya Msingi Mtundu iliyopo Kata ya Mahole Same.

Akizungumza baada ya kuchangia fedha hizo, Kilango amesema shule zinazohitaji  ujenzi zipo nyingi katika  jimbo lake   na shule nyingine tayari  Rais Dk. Samia Suluhu Hassani ameshazijenga na tayari watoto wameingia darasani.

Akielezea fedha alizotoa amesema  zitasaidia kuanza ujenzi wa madarasa matatu na ofisi moja katika shule ya Msingi Mtundu na Serikali Kuu   imehaidi kusaidia ujenzi huo ili madarasa yakamilike kwa wakati.

Aidha amewapongeza  wananchi wa Kata ya Mahole kwa juhudi binafsi katika nyanja mbalimbali za maendeleo hasa eneo la elimu.

"Hapa ninapozungumza tayari wananchi hawa kwa nguvu zao wamejenga Msingi wa madarasa mawili  kwa hatua za maandalizi ya ujenzi wa awali bila kusubiri serikali, "amesema Kilango.

Mbali ya mchango huo zaidi Kilango amewatia moyo wananchi hao kuendelea na mshikamano huo kwa kuhakikisha wanasonga mbele katika kufanikisha shabaha iliyopo ya ujenzi wa ofisi na madarasa Matatu ya Shule ya Mtundu

Amewataka wananchi wa Kata ya Mahole kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kazi kubwa anayoifanya hasa Katika kuleta Maendeleo kwenye Taifa letu 

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mahole Issa Rashid amempongeza Kilango kwa jitihada zake zote kupambana katika kushiriki katika ujenzi huo na kwamba hiyo  inawapa moyo wananchi kuendelea kuchangia ujenzi huo.

Amesema Mbunge wao  ametuonesha upendo wa dhati kwa watoto wetu na Sisi tutaendelea kushirikiana naye bega kwa bega hasa Katika kuleta maendeleo katika jimbo hilo.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...