Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva ameagiza mpaka kufikia Jumatatu ya tarehe 15 mwezi huu wazazi wote wenye watoto wanaotakiwa kuanza Kidato cha kwanza, Darasa la kwanza na Awali kuhakikisha wanawapeleka shuleni watoto hao kuanza masomo haraka iwezekanavyo kwani timu yake itakapopita kukagua na kuwakuta watoto hao majumbani hakutakuwa na muamana na mtu.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa tamko hilo alipofanya ziara ya kutembelea shule mbalimbali wilayani humo ili kuona kasi ya watoto kidato cha kwanza, darasa la kwanza na awali ambao tayari wameripoti ndani ya wiki moja ya ufunguzi wa shule na kukuta idadi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza bado hairidhishi ambapo kwa Wilaya nzima wameripoti asilimia 60 pekee hiku asilimia 40 wakiwa bado hawajatipoti huku kwa darasa la kwanza na awali wakitipoti zaidi ya asilimia 85.

Mwanziva amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka nguvu katika kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa na madawati hivyo wazazi wanapaswa kuungana na serikali katika kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shuleni ili waweze kupata elimu iliyo bora.

"Nimesikia wazazi wanasubiri siku za ya mnada/guluo ili wawanunulie watoto wao mahitaji na kuwaleta shuleni, sasa wiki hii ndiyo wiki ya mnada katika maeneo mbalimbali ya Wilaya yetu- wajitahidi wakamilishe mahitaji, na kwa wale watakaokwama sisi hatuna kipingamizi au masharti yoyote tunachotizama ni watoto kuripoti mashuleni kwanza, ninaomba kwanzia Jumatatu ya Tarehe 15 January kila mtoto awe ameripoti shuleni kuanza masomo".
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...