MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro  Kasilda Mgeni ameongoza wakazi wa wilaya hiyo katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria wilayani humo na kusisitiza usimamizi wa sheria katika kulinda mazingira hasa maeneo yaliyo hifadhiwa.

 Akizungumzia Wiki ya Sheria,  Mgeni amesema wilaya ya Same ni kati ya maeneo yaliyoathiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu na kusababisha kukosa mvua kwa miaka mitatu mfululizo.

Hat hivyo mvua kubwa zilizonyesha pia mwaka huu zimeleta madhara makubwa ikiwemo uharibifu wa miundombinu, Mazao mashambani na baadhi ya makazi ya watu kuharibiwa ikisababishwa na athari za kukithiri kwa shughuli za kikibadamu kwenye maeneo ambayo yaliyopashwa kuhifadhiwa.

“Pamoja na shughuli yenyewe kutoa elimu ya sheria, mmefanya jambo moja la msingi sana ambalo sasa ni kaulimbiu yetu wilaya ya Same ya kuhakikisha tunapanda miti na kuifanya wilaya inakua ya kijani naomba mtumie sheria mnazo zisimamia kuhakikisha miti inalindwa”.

“Kesi zinapokuja kwenu zinazohusiana na masuala ya uharibifu wa mazingira,  naomba mzitilie mkazo sana kwa sababu wilaya yetu imepitia kipindi kigumu cha kukosa mvua miaka mitatu mfululizo na ndio maana tumeamua kuwekea kipaumbele uala hili la kupanda miti na kuitunza, "amesema.

Amewataka pia wakazi wa wilaya hiyo kutumia kipindi chote cha maadhimisho kupata elimu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria kwakua asilimia kubwa ya watu wamekua wakikosa haki zao kwa kutojua sheria, suala ambalo serikali imeona kuja na utaratibu wa kuadhimishwa wiki ya sheri kujenga ukaribu baina ya wataalam na jamii.

Awali Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Same Chrisanta Chitanda amesema maadhimisho hayo yalianza mapema tangu Januari 24 kwa kutoa elimu kupitia mabanda ya maonesho,mikutano mbalimbali na kutembelea maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo Shuleni, shughuli ambazo ni endelevu hadi siku ya kilele februari Mosi mwaka huu 2024.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...