




Na.Mwandishi Wetu-SINGIDA
Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Singida kimeishukuru Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi wake 100 wa fani ya Mifumo ya umeme.
Msajili wa Chuo hicho, Bw. Gelshom Maloda ameiomba EWURA kuendesha mafunzo ya mara kwa ili kuwajengea uwezo wanafunzi katika masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya sekta ya umeme.
Mhandisi mwandamizi Wa Umeme EWURA Kanda ya Kati, Nicholaus Kayombo, amewasilisha mada kuhusu masuala ya msingi ya Mifumo ya Umeme na Madaraja ya leseni za EWURA na namna ya kuomba leseni hizo kwa mtandao kupitia mfumo wa LOIS . Mfumo huo unapatikana katika tovuti ya Mamlaka www.ewura.go.tz.
Wanafunzi wamesisitiziwa umuhimu wa kumiliki leseni zinazotolewa na EWURA, ikiwa ni pamoja na utambulisho wa utalaamu wao, ubora wa huduma na usalama wa mali, watu na mazingira.
Mafunzo hayo yaliyofanyika leo tarehe 29/1/2024, yameratibiwa na EWURA Kanda ya Kati, inayohudumia mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa na Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...