OR-TAMISEMI 

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Wilson Charles amewataka watalaamu wa afya mkoani Mwanza kuimarisha na kuboresha utekelezaji wa mikakati na afua za kudhibiti Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Dkt.Charles ameyasema hayo Januari 21, 2024 alipofanya mkoani humo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa afua mbalimbali za kukabiliana na Mlipuko wa ugonjwa huo  unaoendelea katika Halmashauri za Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemela, Magu na Ukerewe. 

Katika ziara yake, Naibu Katibu Mkuu huyo amekutana na viongozi mbalimbali wa Mkoa na kushiriki katika kikao cha kamati ya kitaalamu cha sekta zote cha kila siku asubuhi ambapo alipata taarifa fupi ya mwenendo wa mlipuko na utekelezaji wa afua za udhibiti na baada ya kupokea taarifa hizo ametoa maelekezo mbalimbali ikiwamo kuimarisha utekelezaji wa afua za kudhibiti ugonjwa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...