Katika picha ni Muasisi wa Huduma ya Ngurumo ya Upako Duniani Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Muasisi wa Huduma ya Ngurumo ya Upako Duniani Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie jumapili ya tarehe 31/12/2023 katika ibada ya Uvuvio wa kuvuka mwaka ametoa Neno la Kinabiia lisemalo Panda ''Viwango Ongeza Thamani ''huku likiwa na Kauli Mbiu isemayo ''Jenga Uwezo'' Neno ambalo waumini hao watatembea nalo kwa mwaka mzima kama dira

Akizungumza katika jumapili ya mwisho wa mwaka amesema kwamba ni utaratibu ambao amekuwa akiongozwa na Mungu kutoa Neno la Kinabii ambalo ni mwongozo kwa yeyote aliyetayari kulishika na kulitendea kazi katika hatua ya Imani.

Awali akihUbiri katika ibada hiyo ya uvuvio Dkt.GeorDavie aliweza kuwaelekeza\ waumini katika huduma hiyo mambo ya muhimu ya kuzingatia katika mwaka 2024, ikiwa ni pamoja na kuacha mizigo yeyote chakavu isoyoleta tija maishani mwao,pamoja na kuachana na mambo ya kale nayoleta michosho,badala yake ufikie wakati wa kukagua marafiki sahihi wenye uwezo wa kuongeza thamani maishani mwao sambamba na kukamata mafundisho yenye viwango.

"Kuna watu wanakuja maishani mwa watu kwaajili ya kuzuia baraka hivyo ni lazima mtu aamue kupanda viwango na kuchukia historia ya kale na kupiga hatua mpya maishani,ili uweze kumiliki baraka,lazima uamue kwamba unataka kufanya mambo ya kihistoria,Nenda na watu wanaoongeza thamani maishani mwako ,Achana na marafiki wasiokuwa na msimamo na wenye fikra hasi mawazo chakavu na asiyekuwa na vision " alisema Dkt. GeorDavie

Aidha aliwataka waumini hao kutambua kuwa zipo baraka ambazo mtu hawezi kuzipokea hadi apande viwango ili thamani ya maisha iweze kuongezeka,huku akiwataka kuachana na mambo na maneno ya kukatisha tamaa badala yake wabakie na watu wanaowaelewa wenye nia safi na kupunguza vitu vinavyozuia kasi yao ya kukua na kuongeza thamani .

''Ukisoma maandiko kutoka kwenye Bibia Takatifu katika Injili YA Luka 5;36-39 ipo wazi kabisa kwamba hakuna akataye kiraka cha vazi jipya na kuweka katika vazi kuukuu,na kama akitia,amelikata lile jipya na kile kiraka cha vazi jipya hakilingani na lile vazi kuukuu''alisema Dkt.GeorDavie.

Sambamba na hayo aliweza kuwasisitiza waumini katika ibada hiyo ya uvuvio kuachana na makundi yanayowatoa nje ya mstari,pamoja na kuwaepuka watu ambao wanaweza kuvunja brand zao bila kujali wametumia muda kiasi gani kwaajili ya kuijenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...