Serikali yatoa wito kutembea Makumbusho ya Jiolojia Tanzania

Zaidi ya wanafunzi 20 wa darasa la tatu kutoka shule ya msingi Reader Rabbit, Bay bridge iliyopo jijini Dar es Salaam wamefika Makumbusho ya Taifa ya Jiolojia Tanzania ili kujifunza Jiolojia ya Miamba na Madini yapatikanayo Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Mafunzo hayo yametokewa leo Januari 31, 2024 na Wataalamu wa Makumbusho hayo kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) baada ya wanafunzi hao kutembea Makumbusho hayo.

Akizunguza katika ziara hiyo, Mwalimu wa shule hiyo ambaye pia ni kiongozi wa timu hiyo Ringo Iringo amefurahishwa na aina za miamba na madini yaliyomo kwenye Makumbusho hayo ambapo amesema wanafunzi wake wamejifunza mengi kuhusina na Jiolojia ya Miamba na Madini yapatikanayo Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Sambamba na hayo Iringo amesema wanafunzi wake wamejifunza Jiolojia ya Tanzania, Afrika na ulimwengu mzima kwa nadhalia hivyo uongozi wa shule hiyo ukaona umuhimu wa kufika katika Makumbusho hayo ili kujifunza kwa vitendo.

Kwa upande wake, Kaimu Msimamizi wa Makumbusho hayo, Andrew Buluba ameipongeza shule hiyo kufika katika Makumbusho hayo kujifunza Jiolojia ya Miamba na Madini ambapo amesema elimu hiyo itawasaidia katika masomo yao hususan somo la Jografia.

Naye, Mjiolojia kutoka GST Berther Matobango, ametoa wito kwa shule nyingine kutembea Makumbusho hayo kwa lengo la kujifunza Jiolojia ya Miamba na Madini yapatikanayo Tanzania, Afrika na ulimwenguni kote.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Kanzi Data ya Taifa ya Jiolojia kutoka GST Renata Bitumbiko amesema, Makumbusho ya Taifa ya Jiolojia Tanzania yalianzishwa na Mamlaka ya Utawala wa Makoloni ya nje ya Serikali ya Kikoloni ya Muingereza mnamo mwaka 2025 kwa lengo la kukusanya na kuhifadhi sampuli za miamba na madini ili kusaidia kuonesha aina za madini zilizopo katika himaya fulani na kusaidia wataalamu kufanya marejeo.

Akitoa maelezo kuhusu Makumbusho hayo, Mjiolojia kutoka GST Mustadi Shabani amesema Makumbusho hayo yalikusudia kuonesha Jiolojia na rasilimali madini iliyopo nchini na kuwapa mwelekeo washimbaji na watafutaji wa madini katika maeneo mbalimbali kwa maendeleo ya nchi.

Vision2030MadininiMaishanaUtajiriMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...