Jumla ya vifo 2,648 vinavyotokana na uzazi vimeweza kuzuiwa katika mikoa 10 nchini huku serikali ikiendelea na mikakati kudhibiti matukio ya utoaji mimba wakati takwimu zikionesha mpaka sasa kuna matukio 458,139 ya utoaji mimba usio salama.

Kupitia mradi wa WISH 2 ACTION wenye lengo la kuchochea mabadiliko ya afya ya uzazi, serikali imefanikiwa kuepusha mimba zisizotarajiwa zaidi ya mimba milioni 1.6 katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma,Mara,Rukwa,Ruvuma Njombe, katavi na Mbeya.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UMATI Suzana Mkanzabi, wakati alipowakutanisha wadau wote waliofanikisha utekelezaji wa mradi huo, kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza.

Alisema kuwa jumla ya watu milioni 3.8 wamepatiwa huduma za afya ya uzazi na vituo vya afya takribani 300 vimepatiwa vifaa tiba kupitia mradi huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Afya wa Shirika la Marie Stopes Dk Geofrey Sigalla alisema mradi huo umelenga kumkomboa mwananchi hasa anaetoka kaya maskini katika maeneo ya uzazi wa mpango, maambukizi ya Ukimwi na kukinga saratani ya kizazi kwa wanawake.

Pamoja na mambo mengine Dk Sigalla aliiomba serikali kujikita katika kutatua changamoto maeneo mtambuka ikiwemo kuwezesha vituo vya afya kutoa huduma himilivu kama vile kuongeza vitendea kazi, pamoja na kuwa na uwezo wa kuwafikia wateja.

Mratibu wa Huduma ya Mama na Mtoto kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Dk Yahya Hussein alisema mradi wa kutoa elimu ya afya ya uzazi utaendelezwa na serikali kutokana na mafanikio yake.

Tanzania kama nchi zingine duniani inatekeleza Malengo endelevu wa Dunia SDGs inayotaka kila nchi mwanachama kupunguza vifo vitokavyo na uzazi kufikia vifo 70 kwa kila vizazi hai 100,000.


 

Mkurugenzi mtendaji wa UMAT,Bi Suzana Mkanzabi akitoa taarfa ya mradi wa WISH 2 ACTION katika mkutano na wadau wa Afya ya Uzazi
 

Mkurugenzi wa huduma za Afya,Shirika la Marie Stopes ,Dkt Geofrey Sigalla akizungumza na waandishi wa Habari
 

Picha ya Pamoja ya Washiriki katika mkutano wa wadau wa Afya ya Uzazi
 

Mratibu wa huduma ya Mama na mtoto Dkt. Phineas Sospeter kutoka wizara ya afya akizungumza na wadau wa Afya ya uzazi waliojitokeza katika hafla hiyo
 

Baadhi ya Washiriki wakitoa maoni yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...