Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeendesha semina kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) leo tarehe 27 Januari, 2024 jijini Dodoma.
Semina hiyo imelenga kuwapa uelewa Wabunge wa Kamati ya PIC juu ya Uwekezaji na mwenendo wa sekta hiyo nchini pamoja na kufahamu mikakati mbalimbali inayotekelezwa na TIC katika kuimarisha sekta hiyo na kuhamasisha zaidi uwekezaji.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe Deus Clement Sangu (Mb), ameipongeza TIC kwa kuendesha semina hiyo iliyotoa fursa kwa wajumbe hao kufahamu zaidi juu ya uratibu wa uwekezaji nchini na kufahamu kwa hali halisi ya uwekezaji, malengo, fursa na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dkt. Binilith Mahenge, amewapongeza wajumbe wa Kamati ya PIC kwa kazi nzuri wanayofanya na ushirikiano wanaoutoa katika kusaidia kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya TIC.
Semina hiyo pia imehudhuriwa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uwekezaji- Sekta Binafsi wa Wizara ya Ndg. Fadhili Chilumba na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya TIC ambao ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Ndg. Shani Mayosa, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Ndg. Pascal Maganga na Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji Ndg. John Mnali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Deus Sangu akizungumza katika Semina iliyoandaliwa na TIC kwa Wabunge wa Kamati hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa bodi ya TIC Dkt. Binilith Mahenge akizungumza wakati wa semina kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji -TIC John Mnali akitoa maelezo kuhusiana na uhamasishaji wakati wa semina kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uwekezaji- Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Fadhili Chilumba akitoa mada wakati wa semina kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya matukio ya Picha katika Semina ya Kamati ya Bunge iliyoratibiwa na TIC
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...