Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti na Uchumi wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Daniel Sillo (mbele) kukagua mabwawa ya maji ya mradi wa Butimba, jana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Bajeti na Uchumi, Daniel Sillo, akipanda mti katika chanzo cha Maji Butimba baada ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa mradi huo jana.


Na BALTAZAR MASHAKA,MWANZA
KAMATI ya Kudumu ya Bunge,Bajeti na Uchumi imesema,haitakuwa kikwazo cha miradi ya maji ya kuhudumia wananchi inayotekelezwa na mipya itakayoanzishwa na serikali huku ikieleza mradi wa Butimba utamaliza changamoto ya maji mkoani Mwanza.


Kauli hiyo ilitolewa leo jijini Mwanza na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Daniel Sillo baada ya kutembelea ujenzi wa Mradi wa Chanzo kipya cha Maji na Kituo cha Tiba ya Maji Butimba,kinachojengwa kwa gharama ya sh.bilioni 82.


Amesema Kamati ya Bunge ya Bajeti na Uchumi imeridhishwa na utekekezaji wa mradi huo wa Maji Butimba,na hivyo haitakuwa kikwazo kwa miradi mingine ya maji iliyopo na mipya itakayoanzishwa na serikali ili kuwaondolea wananchi changamoto ya ukosefu wa maji.


Sillo amesema wajumbe wameridhika na mradi huo mkubwa wa maji wa Butimba,utakapokamilika utapunguza changamoto ya mgawo na uhaba wa maji kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na wilaya jirani kama si kuumaliza kabisa.


Amesema kamati hiyo itaendelea kukaa na kuishauri serikali kutenga fedha za kutosha kutekeleza miradi hiyo ikiwemo ambayo haijawahi kupata fedha ili kutatua kero ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwa Watanzania.


"Sisi kamati kazi yetu ni kutenga fedha za miradi ya sekta zote za kiuchumi ikiwemo miradi muhimu ya maji,hatutakuwa kikwazo kwa miradi mingine inayoendelea hata ile mipya itakayoibuliwa katika maeneo mbalimbali,”amesema Sillo na kuongeza;


“Kamati imeridhika na Mradi huu wa Butimba unaotekelezwa na Wizara ya Maji na tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,kwa dhamira yake ya kutoka fedha ili kumtua mama ndoo kichwani,changamoto ambayo ni ya muda mrefu katika Jiji na Mkoa wa Mwanza."


Mbunge huyo wa Babati (CCM) mkoani Manyara amesema mradi huo uliogharimu sh.bilioni 82 sawa na Euro milioni 131,ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM,utakapokamilika utatatua changamoto ya uhaba wa maji safi na salama mahitaji ya lita milioni 172 kwa wakazi wa jiji na maeneo ya pembezoni.


Kwa upande wake Waziri wa Maji,Jumaa Aweso amesema wizara hiyo iligeuka kuwa ya kero,moja ikiwa ni changamoto ya upatikanaji wa fedha za miradi ya maji sababu ya ufinyu wa bajeti na mingine haikuwahi kupata fedha tangu mwaka 1980.


Ameigiza MWAUWASA kuwa kukamilika kwa mradi wa Butimba uliofikia asilimia 99 kusiwepo sababu ya watu kutounganishwa na huduma hiyo,watu waunganishwe kwa muda mfupi wapate maji safi na salama ya kutosha na kuipongeza Bodi,Menejeimenti na watalaamu kwa usimamizi mzuri wa mradi huo.


Mbunge huyo wa Pangani (CCM) amesema uelekeo wa wizara ni ujenzi wa miradi ya kimkakati katika maeneo ya miji 28 yenye changamoto kubwa yaliyoanishwa ili kutatua kero hiyo kwa kutumia chanzo toshelevu na kila eneo lina mkandarasi katika miradi hiyo.


“Tunatumia chanzo toshelevu kuhakikisha tunatatua changamoto ya maji na tumepewa maelekezo na Rais ifikapo 2025 upatikanaji wa maji vijijini uwe umefikia asilimia 85 na mijini asilimia 95 na hadi sasa mijini wana asimilia 88 na vijijini asilimia 77,”ameeleza Aweso.


Waziri huyo wa Maji amesema wana miradi zaidi ya 244 mijini ambayo ikikamilika watafikia hiyo asilimia 95 ya upatikanaji wa maji pia,vijijini wanatekeleza miradi zaidi ya 1500 na mkakati ni kuhakikisha wanaisimamia na kukamilika kwa wakati ili kufikisha asilimia 85.


Kwa mujibu wa Aweso vijiji 2000 vinapata maji siyo ya uhakika ambapo Rais Dk.Samia aliipatia mikoa yote magari ya vifaa vya kisasa vya kuchimba visima na hivyo hategemei wahandisi wa mikoa ama wilaya vijiji vikose maji ilhali magari yapo wameyaegesha,lazima yatumike kuchimba visima na watu wapate huduma ya maji safi na salama.


Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, CPA Amos Makalla ameieleza Kamati ya Bunge ya Bajeti na Uchumi kuwa Mwanza ilikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa miaka mingi tangu akiwa Naibu Waziri wa Maji ambapo serikali ilipata malalamiko ya wananchi kwa nini wakose maji wakati Ziwa Viktoria liko karibu.


“Mahitaji yalikuwa lita za maji zaidi ya lita 167 kwa siku,chanzo cha Capripoint kikizalisha lita milioni 90 na hivyo kusababisha upungufu na mgawo wa maji.Rais alifanya maamuzi ya kutoa fedha za mradi wa Butimba na leo nafarijika unakwenda kukamilika kwa asilimia 100 ukiwa na mitambo ya kuzalisha lita milioni 148,mgawo utapungua,”amesema.Meneja Miradi wa MWAUWASA Celestine Mahubi amesema mradi huo una hatua nne za kuchukua maji ziwani na kuyapeleka katika mtambo na kisha kusukuma kwenye matenki na kisha kuyasambaza kwa wananchi ambapo bomba la urefu wa kilomita moja limelazwa katika chanzo cha maji majini hadi nchi kavu.
wenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Bajeti na Uchumi, Daniel Sillo, akibonyeza kasa ya mashine Tarakishi (Kompyuta) kuwasha mtambo wa kutibu maji wa mradi wa Butimba, jana kamati hiyo ilipokagua ujenzi wa mradi huo uliogharimu Euro milioni 131 sawa na sh. bilioni 82 za Kitanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...