Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara ametembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambapo amepata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

Prof. Kahyarara aliyeambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi alipokelewa na Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA Bw. Teophory Mbilinyi ambapo alimpatia maelezo juu ya mradi huo Pamoja na kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.

Kwa upande wake Profesa Kahyarara ameipongeza TCAA kwa usimamizi mzuri wa Sekta ya Usafiri wa Anga na kuahidi serikali itaendelea kuwekeza katika sekta hii muhimu pia alisisitiza chuo kuendelea kujitangaza zaidi ili kisikike na kuwafikia watu wengi Zaidi ndani na nje ya nchi.

Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akizungumza jambo kwenye Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) alipoambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi walipotembelea Banda la TCAA  kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara pamoja Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA Bw. Teophory Mbilinyi  kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo pamoja na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) walipotembelea Banda la TCAA  kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara  akisaini kitabu katika Banda Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi 
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA Bw. Teophory Mbilinyi  mara baada ya kutembelea Banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA Bw. Teophory Mbilinyi  mara baada ya kutembelea Banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara  pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi  wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...