Na. WAF - Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Suala la Lishe ni jambo kubwa ambalo limepewa kipaumbele katika Sekta ya Afya kwa kuwa ni ajenda kubwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Ummy amesema hayo leo Januari 11, 2023 alipokutana na watumishi wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) baada ya kutolewa tamko la kufutwa kwa Taasisi hiyo na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina.

“Ajenda hii ya lishe ni ajenda muhimu sana kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hii ni ajenda yake ambayo anaipa kipaumbele cha juu na sisi kama Wizara ni kipaumbele chetu.” Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema hakuna mtumishi yoyote wa Taasisi hiyo atakae poteza haki zake na stahiki zake za msingi ikiwemo kazi na stahiki nyinginezo.

“Kazi kubwa tunayoifanya sasa ni kujadiliana namna bora zaidi ya kuendelea kusimamia masuala ya Lishe ndani ya Wizara na pia ndani ya Serikali kwa ujumla. Waziri Ummy ameeleza kuwa kwa sasa jina la TFNC litaendelea kutumika hadi itakavyoelekezwa vinginenyo, kinachobadilika hapo ni hali ya kisheria ‘legal status’.”

Mwisho, Waziri Ummy amesema kuwa kazi na majukumu ya Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) yataendelea kama kawaida kwa kutumia bajeti yao ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Waziri Ummy ameambatana na timu kutoka Wizara ya Afya akiwemo Katibu Mkuu Dkt. John Jingu, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Grace Magembe pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...