MBUNGE wa Jimbo la Kalenga lililopo Mkoa wa Iringa Jackson Kiswaga amekabidhi jumla ya mifuko 30 ya Saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya Msingi Kiwere iliyopo Jimboni hapo.

UJENZI wa madarasa haya mapya unatokana na shule hiyo kuzidiwa na idadi kubwa ya Wanafunzi na kupelekea Darasa moja kusoma Wanafunzi zaidi ya 100 jambo linaloathili ufaulu wao.

"Nia ya serikali ni kuhakikisha kila mwanafunzi anasoma katika hali nzuri darasa moja kuwa na Wanafunzi wengi hii inaweza kuathili ufaulu hivyo tutashirikiana kwa pamoja hadi kukamilika kwa madarasa haya na kama Mbunge nitaendelea kuikumbusha serikali ili itusaidie Ile Milioni 175 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa" Amesema Kiswaga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...