Na Mwandishi Wetu
MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga, ameomba, wadau, taasisi na mashirika kuendelea kutoa misaada kwa wa athirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha mkoani humo.
Amesema mvua hiyo pia imelazim Shule ya Sekondari Juhudi iliyopo katika halmashauri hiyo kufungwa kutokana na kuzingirwa na maji na kufanya uongozi kutafuta eneo lingine la kujenga shule hiyo.
Meya Kihanga amesema kata nne za Lukobe, Kihonda, Mkundi na Mazimbu, zimeathirika kwa kiasai kikubwa na mafuriko hayo.
Ametaja kata zingine zilizoathiriwa na mvuaa hiyo ni Mindu na Bigwa ambazo licha ya kutokuaathirika sana lakini misaada ya hali na mali inahitajika.
“Kuna hali ngumu kwa wananchi katika maeneo hayo. Nyumba nyingi zimebomoka, zimeingiliwa na maji na kusomba mali za wananchi. Wengi hawana paa kuishi, chakula na mavazi,”amesema Meya Kihanga.
Ameeleza, kutokana athari hizo hatua mbalimbali zimechukuliwa na serikali ya mkoa,wilaya na halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi waliokosa mahari pa kuishi wanahifadhiwa, kupatiwa chakula na mavazi.
“Sisi mpaka sasa tumeanza kutoa misaada mbalimbali kwa uwezo wetu. Ninaiomba jamii, ituangalie Morogoro kama inavyo ziangalia sehemu zingine zilizoaathiriwa na mafuriko. Tunahitaji misaada,”amesema.
Amebainisha mahitaji yanayohitajika zaidi ni chakula, mavazi, magodorona mashuka na misaada yote ikabidhiwe Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
Amesemaa misaada inapokelewa kutoka kwa mtu yoyote, mkoa wowote na hata akiwa na mavazi mazuri yaliyovaliwa.
Meya Kihanga, amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari hasa wakati huu mvua inapoendelea kunyesha.
“Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekuwa ikitoa tahaadhari ya kuwepo kwa mvua zaidi. Wananchi wachukue tahadhari.Pia walinde watoto na kuto kudharau nguvu ya maji,”ameeleza Meya Kihanga.
Ameishukuru Serikali hususan Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama, ambaye amekuwa mstari wa mbele kushughulikia athari hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...