Na John Walter-Babati.

Walimu wametakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia maadili kwa wanafunzi mashuleni ili kuwa na kizazi bora baadaye.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Babati Vijijini Daniel Sillo alipokutana na wakuu wa shule za msingi Halmashauri ya wilaya ya Babati kujadili kujadili changamoto zinazowakabili na kuangalia namna bora ya kuendelea kuboresha hali ya elimu kwa mwaka 2024.

Sillo amewahakikishia Walimu kuwa changamoto zote zilizo ndani ya uwezo wake atazitatua na zingine ataziwasilisha sehemu husika ili Serikali ya chama cha Mapinduzi izifanyie kazi.

Aidha amewataka waalimu kutekeleza majukumu yao ili kuitendea haki serikali iliyowapa madaraka na kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo.
Sillo ametoa motisha kwa walimu hao kwa kuwapa mitungi ya gesi akiwahamasisha kuendelea kuielimisha jamii umuhimu wa kutumia nishati mabadala kuepuka uharibifu wa mazingira kupitia matumizi mkaa na kuni.

Naye Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema serikali itaendelea kuwa karibu na walimu muda wote huku akiwasisitiza kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsi kwa kuzungumza na wanafunzi mara kwa mara pamoja kuitisha vikao vya wazazi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu wa shule za Msingi Tanzania wilaya ya Babati Selemani Adam amempongeza na kumshukuru Mbunge Sillo kwa kuwapatia mitungi hiyo pamoja na kuwawakilisha vyema wananchi wote bila kujali vyeo vyao.

Sillo amekutana na Walimu hao ikiwa imebaki Siku moja kabla ya shule za msingi na Sekondari nchini kufunguliwa kwa muhula mpya wa masomo.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...