-Mtendaji wa kijiji afunguka mbele ya mbunge Mwanyika kutamani kuchoma cheti kisa kutopandishwa daraja "Nilitamani nikipige kiberiti kwasababu hakina kazi"


Njombe

Baadhi ya watumishi wa serikali katika halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe wamelalamikia kitendo cha kutopanda madaraja na vyeo licha ya kufanya kazi kwa muda mrefu na kuongeza kiwango cha elimu.

Wameto kilio chao kwenye mkutano uliyoitishwa na mbunge wa jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika wenye lengo la kusikiliza changamoto zinazowakumba watumishi kutoka kada tofauti katika utekelezaji wa majukumu yao,watumishi hao akiwemo Musa Lutiginga wamesema kitendo  cha kuongeza elimu na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupanda vyeo na mishahara kunavunja moyo hadi inafika wakati wanatamani kuchoma moto vyeti vya elimu walizo ongeza huku pia wakiomba swala la kikokotoo kupitiwa upya kwa kuwa kinaumiza watumishi

"Mfano mtu amemaliza diploma anakuja kuonyesha cheti wanasema ulichoajiliwa nacho utabakiwa nacho kingine hawakitambui kuna siku nilitamani nikipige moto au nikichane kwasababu hakina kazi yoyote na kila nikiwasilisha wanasema sisi tunachotambua na hiki na ndio maana watu wanaona kwenda kusoma haina maana"amesema Musa Lutiginga mtendaji wa kijiji cha Igoma

Paul Mwansansu ni kaimu afisa Utumishi halmashauri ya mji Njombe kwa niaba ya mkurugenzi ametoa ufafanuzi juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali ili kutatua changamoto hiyo

"Changamoto ya upandishwaji madaraja au vyeo kwa upande wa watumishi ilikuwa ni kubwa sana hasa kipindi cha mwaka 2015-2016 kutokana na uhakiki uliokuwa unafanyika kwa hiyo kutokana na hili kama kuna mtu bado ana kesi ya kipekee anatakiwa afike kwenye ofisi ya utumishi na kuandika mtililiko wote ili tulichambue kabla ya kumuandikia barua katibu mkuu utumishi"amesema Mwansansu

Mara baada ya kupokea kero mbalimbali ikiwemo ya kikokotoo na upandaji wa madaraja kwa watumishi Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika amesema suala hilo wanakwenda kuliwasilisha katika vikao vya bunge kwakuwa lina maslahi na kundi kubwa.

"Inawezekanaje unakwenda kusoma halafu unarudi unaambiwa huwezi kupata cheo mpaka utumikie cheo kazi kwa hiyo wenzetu wana maelekezo tayari wanatakiwa wayafanyie kazi na mapema sana kama kutakuwa bado kuna waathirika basi tupewe taarifa mapema"amesema Mwanyika
 
Mbunge Mwanyika anaendelea na ziara ya kikazi jimboni kwake ya kusikiliza kero za wananchi na kutoa mrejesho wa utekelezaji wa ilani ya chama katika miradi ya maendeleo.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...